Nisaidieni jinsi ya kufunga kampuni

Nisaidieni jinsi ya kufunga kampuni

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,830
Reaction score
4,729
Mambo zenu,

Nataka kufunga kampuni baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa biashara, anayejua process anipe fasta. Haina deni na documents zote ziko okay. Naanzia wapi na naishia wapi?

Karibuni
 
Andika barua kuelezea idhini yako, ambatanisha na vielelezo vyote kwenda taasisi zoote ulizopitia kipindi unaanzisha kampuni,

Kuanzia manispaa, TRA, Blera n.k

Note: hakikisha kote huko unakopeleka barua unakwenda na copy 2 moja unasubmit nyingine inapigwa muhuri wa masijala unabaki nayo kama reference

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni huwa haifungwi labda kudeclare imefilisika ambapo mchakato wake lazima uajili kampuni nyingine ya kuifilisi lakini itaendelea kuexist Brela na TRA na account yake benki itaendelea kuwepo lakini kuwa inactive kama ilishafanya biashara! Pia kama iyo kampuni ilikuwa limited company na inashare holders sio rahisi kivile Labda cha kufanya ni kwenda Brela watakupa mwongozo ambao utahusisha TRA kuhusu hizo hisa.
 
No retreat no surrender,
Njia Bora zaidi ni kumuuzia mtu kampuni hio iwapo haina madeni,records zako zote ziko vizuri,na mambo yote ya kikampuni yako vizuri.Je kampuni yako inamuda gani tangu uisajili na ilikuwa inafanya shughuli gani?Share capital ni kiasi gani?Kuna assets zozote ambazo ziko kwa jina la kampuni?Nijibu hata PM kuna watu wanaweza wakahitaji kampuni ya namna hio ambayo imesajiliwa muda mrefu.
 
Itabidi utangaze kwenye gazeti ili kutoa nafasi kwa mwenye pingamizi kama madeni na hapo uwe tayari umeshafanya tax clearance na Brella hawakudai watakupa go ahead,sio rahisi kufunga kampuni ambao ni limited maana itabidi uwe na resolution ya board ndio upeleke brella na Tra.ukimaliza process za tra na brela ndio utatangaza kwenye magazeti,kama kampuni ni kubwa utahitaji kuwa na liquidator atakayesimamia madeni yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti ya kuuza na kufunga hamna kwani unachofanya ni kujiondoa katika ownership na kumpatia mtu mwingine umiliki.Ila kama unataka kuifunga kwa muda kisha baadae uifungue basi nenda brela na TRA unawajulisha kwamba You have Seized Trading.
Hiyo itakuwa safi zaidi naweza kusimamisha kwa miaka hata 10?
 
Hiyo itakuwa safi zaidi naweza kusimamisha kwa miaka hata 10?
Miaka 10 mingi, maana itabidi uendelee kulipia baadhi ya mambo kila mwaka kule BRELA.Kama umeamua basi itabidi ufanye winding up to,Ongea na Mwanasheria akuongoze ili isikuletee usumbufu
 
Miaka 10 mingi, maana itabidi uendelee kulipia baadhi ya mambo kila mwaka kule BRELA.Kama umeamua basi itabidi ufanye winding up to,Ongea na Mwanasheria akuongoze ili isikuletee usumbufu
Na vipi endapo utaamua kutelekeza kimya kimya bila kutoa info popote
 
Mambo zenu,

Nataka kufunga kampuni baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa biashara, anayejua process anipe fasta. Haina deni na documents zote ziko okay. Naanzia wapi na naishia wapi?

Karibuni
Unafunga biashara wakati mzee meko anasema uchumi unakua? jiandae kuambiwa ulikua mpiga dili!

NB: Kuna memba humu anaujuzi na haya mambo nimesahau jina lake ana uzi flani hivi anaelezeaga mambo ya kodi...

Unachotakiwa kujua usipofwata taratibu kufunga kuna siku utarudi na utapigiwa hesabu za kodi mpaka utashangaa! Hakikisha unafwata taratibu zote za kufunga biashara.

Cc Magufuli rais wa wanyonge.
 
Back
Top Bottom