Nisaidieni kumpa jina

lidoda

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2008
Posts
641
Reaction score
574
naishukuru sana jf na zaidi zaidi jukwaa hili. Nashukuru sababu jf imenisidia kupata mke na tunatarajia kupata tunda letu la ndoa hivi kalibuni. Sasa kwa kutoa shukrani na kumbukumbu ya kumpa jina mtoto wetu tumefikiria majina yafuatayo. Kama atakuwa ni mtoto wa kiume tutampajina jamii na kama atakuwa ni wa kike tutampa jina jamia.
Hata hivyo tunatoa fursa ya wanajamii kupendekeza majina ya mtoto mtarajiwa.
Nawasilisha
 
Mhh hongera kwa hilo na hongera kwa kujaliwa kukpata mke na kujaliwa vile vile ujauuzito huo
Mungu awajalie kila la heri kuweza kufikia mwisho mwema
 
Hongereni ila ningeshauri majina mchague wenyewe, au muombe ndugu na marafiki zenu wa karibu wawasaidie.
 
Ushauri wangu hebu kaeni wenyewe kama mke na mume mchague jina la mtoto wenu msitegemee sana humu
Na ikishindikana watafuteni ndugu
Ila naamini baina yenu wawili hamtashindwa kupata jina
 
mhh hongera kwa hilo na hongera kwa kujaliwa kukpata mke na kujaliwa vile vile ujauuzito huo
mungu awajalie kila la heri kuweza kufikia mwisho mwema

asante sana
 
Mkuu ni mtoto wako bana
hata kama mahusiano yalianzia humu na watu wa humu ndo walikusaidia mpe mtoto jina ambalo unalipenda na wala halina influence ya kitu chochote
Usije ukampa jina kwa kuwa eti JF ndo ulikompata wife wako bana
HAta mtoto ukija kumweleza jina lako linatokana na kumpata mama yako JF sijui atajisikiaje
Mpe jina ambalo wewe na mkeo mmekubaliana na linawapendeza na ambalo mtalifurahia wote
 

He. . .majina gan hayo watoto watataniwa shuleni bure, mfano akiwa wa kike wenzake watalinyumbua linaeza kuwa hata jamii wakaongeza vipachikwa mkia (suffix) kama -ana, -neni, -nishwa tehe tehe,
Fikirieni bwana majina yapo mengi, au ndo nyie kina network rushobozi, kokunokia rweyemamu. Msiwe wavivu kufikiria.
 
jamii?

Jamia

unamuita mtoto jamii? Jamii gani? Unataka madhila yote ya jamii yampate mwanao?

Jamia ina maana gani?

Kama wewe na mkeo mmekosa majina kwa nini msimuite mtoto Rehema, Neema, Baraka au Heri?
 
Mkuu hongera sana kwa kupata mke ana kutegemea mtoto hivikaribuni.
Kama hutajali, naomba nipendekeze majina haya hapa.,

Akiwa wa kiume: Aitwe Mbimbinho
Akiwa wa Kike: Aitwe Mbimbinha

Nitafurahi sana kama mtapokea ushauri wangu...)
 
Nafikili muite majina yafuatayo
Lowasa,Chenge Rostam ni majina mazuri na yamepata umaarufu sana.
 
wa kiume muite jeff (kifupi atajulikana kama JF) teh teh teh
 
wa kike muite Erica,wa kiume mwita brian....usimpe majina ya ajabu ajabu mtoto...lol
 
watu wengine sijui kama huwa mko siriaz? Au mnajua mambo ya msingi?

Mwiteni Mkosajina.
 
Blandina, akiwa wa kike, kama zawadi kwa madaktari waliogoma na kusimamishwa katibu wa wizara ya afya.
 
Kuna jina la Kitanzania halisi ambalo linaweza kutumiwa na yeyote<awe wakiume ama wakike>Mwiteni "MIGOMO".Hata hivyo hongereni na endeleeni kumuomba mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…