Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe bodaboda wa Dodoma mjini halafu huielewi ofisi ya waziri wa mambo ya ndani hapo Dodoma?Habari wakuu, Naandika huu ujumbe kwa maumivu makali sana, kilio simanzi na maumivu yasiyoelezeka,
Nilishawahi kuleta mada hii hapa jukwaani bahati mbaya sana haikupata wadau wengi, haikupata wachangiaji na mwisho wa siku uzi wangu ulifunikwa na nyuzi za vichekesho, vibonzo na stori za kuchekesha hii inaonesha ni kiasi gani Watanzania tusivyochukulia sereous mambo mhimu.
Leo naandika hapa nikiamini hapa jukwaani wapo viongozi mbalimbali au watu mbalimbali ambao wanaweza kuucopy huu ujumbe wangu kisha kumtumia waziri mwenye dhamana ya kulitatua hili au kwa mkuu wa Polisi Tanzania, au hata kuniwekea hapa namba ambayo anapatikana whatsup au email ili nimtumie mimi mwenyewe kero hii pengine hapo anaweza kuitatua.
Ninaamini nchi yangu na viongozi wetu hawana lengo baya kwa vijana na wanainchi wake ila kuna baadhi ya watu wanafanya haya kwa masrahi yao binafsi na chuki zao binafsi kutufanya vijana tuichukie serikali na kuona kama tunaserikali kandamizi na isiyo na huruma kwa wanainchi wake.
Mara nyingi nilishaleta malalamiko ya Polisi Kituo kikuu Dodoma (Dodoma centro police) kuwatesa na kuwanyanyasa madereva bodaboda na hata kuwapiga vijana makofi kwa makosa yasiyokuwa na sababu, na ikiwa bodaboda anakamatwa kwa kosa la trafic case kuna haja gani ya kumpiga kumdhalilisha na hata kutumia lugha za kashfa na matusi kwa kijana ambae anatafta riziki?
Kumekuwa na tabia ya Polisi kukamata bodaboda na kumtaftia makosa mengi kisha kumtoza shilingi elfu kumi kwa kila kosa 10,000/=, hapa utakuta Bodaboda amejumlishiwa makosa 10 na anatakiwa kulipa laki moja,
Sasa hapo kijana wawatu anadaiwa rejesho na boss pikipiki ya mkataba kila siku rejesho, na ikikamatwa kama hana hela hapo pikipiki inaenda kupakiwa kituoni na hapo kijana wawatu haingizi chochote na pikipiki inasoma rejesho zikipita siku5 maboss wanachukua pikipiki yao hapo kijana wawatu kala hasara maana pikipiki za mikataba huwa kuna kiasi wanatanguliza ko ikichukulia hapo kijana kala hasara.
Maana kwa sasa Kituo cha police Dodoma wanategemea mapato kutoka kwa bodaboda, vijana ambao kwa changamoto za kazi zao hata shilingi elfu 10 kwa siku wanaingiza kwa mbinde.
Nizaidieni kusambaza huu ujumbe huu.
Ajabu ipi? Inatakiwa muelekeze hivi mimi kutokutambua kama ilipaswa niandikie mkuu wa wilaya barua sikulitambua lakin pia nje ya kulitambua bado napata mazingira magum namna ya kumfikia na kumkabidhi barua yakeWewe bodaboda wa Dodoma mjini halafu huielewi ofisi ya waziri wa mambo ya ndani hapo Dodoma?
Anza kupeleka malalamiko yako kwa mkuu wa wilaya yako, kama hujasikilizwa nenda kwa mkuu wa mkoa, kama hujasikilizwa nenda kwa waziri.
Au nenda moja kwa moja kwa waziri, usipeleke malalamiko ya mdomo tu kote unakopita, peleka kwa barua pia/ Na uwe na kopi iliyosainiwa na anaeipokea.
Ajabu hii.
Hiyo kopi inasainiwa na nani na barua inapita wapi na wapi hebu nifafanulie niandike maana ni zaidi ya mateso kwa vijana mimi sio bodaboda japokuwa mara nyingi ninatumia usafiri wa pikipiki kwa shughuli zangu na hizi adha wenyeji wa dodoma mjini wote hasa wafanyabiashara na wakazi wa majengo wanaijua vzuri sana,mimi hapa nimejitolea kuwapazia sauti kwa kuwa bodaboda ni maisha niliwahi kupitia hata kabla sijawa katika maisha niliyonayo sasaWewe bodaboda wa Dodoma mjini halafu huielewi ofisi ya waziri wa mambo ya ndani hapo Dodoma?
Anza kupeleka malalamiko yako kwa mkuu wa wilaya yako, kama hujasikilizwa nenda kwa mkuu wa mkoa, kama hujasikilizwa nenda kwa waziri.
Au nenda moja kwa moja kwa waziri, usipeleke malalamiko ya mdomo tu kote unakopita, peleka kwa barua pia/ Na uwe na kopi iliyosainiwa na anaeipokea.
Ajabu hii.
Pole sana.Ajabu ipi? Inatakiwa muelekeze hivi mimi kutokutambua kama ilipaswa niandikie mkuu wa wilaya barua sikulitambua lakin pia nje ya kulitambua bado napata mazingira magum namna ya kumfikia na kumkabidhi barua yake
Hili la polisi ni Tanzania nzima watu wanalalamika. Ndiyo maana kwengine wanjichukulia sheria mkononi kuwatandika na kuwachomea vituo.Hili kweli liangaliwe polisi Dodoma mjini wanakela sana
Wanakera sana aseeHawa jamaa acha tu, ...hapohapo police central Dodoma wana mradi wao mpya huu uko hivi, usiku wakiwa patrol hasa siku zinapochezwa game UEFA champions league zile za late night wanakwenda na karandinga lao maeneo ya mabanda wanakoonesha mpira (hasa mailimbili kwa mudy na chang'ombe) wanalitegesha karandinga mlangoni halafu wanashuka na kuingia ndani ya banda inapigwa ambush wote mnaingia ndani ya karandinga then mnapelekwa central na kuandikiwa makosa ya uzururaji, hapo inabidi muanze taratibu za kutoka kila mtu kivyake, hapo ndipo maokoto yanapoanza na si chini 40k
Usilazimishe kila mmoja kutia neno, maneno mengine huwa yanabomoa!Na inaskitisha kuona uzi wa aina hii ambao umebeba hisia na mioyo ya Vijana watu wanau skip bila kucoment chochote
Sasa mkuu boda boda na ccm si samaki na maji? Mnatumika sana kwenye siasa zao, yakiwakuta ndio mnataka msaada kwa jamii?!! Pambaneni nao tu, hao ni wenzenuTunatafta amani ila kiwamudu najua inawezekana ila tunataka tuishi kwa aman