Nisaidieni kupaza hii sauti iwafikie Wakuu wa Nchi, Sakata la bodaboda Dodoma ni zaidi ya mateso kwa vijana wetu

Bodaboda ni janga la taifa, huwa napata taabu sana kuwatetea hasa kwenye makosa yanayohusu sheria za barabarani. LATRA inabidi waweke sheria kali sana za udhibiti wa Bodaboda ama sivyo tutavuna mabua.
 
Wewe bodaboda wa Dodoma mjini halafu huielewi ofisi ya waziri wa mambo ya ndani hapo Dodoma?

Anza kupeleka malalamiko yako kwa mkuu wa wilaya yako, kama hujasikilizwa nenda kwa mkuu wa mkoa, kama hujasikilizwa nenda kwa waziri.

Au nenda moja kwa moja kwa waziri, usipeleke malalamiko ya mdomo tu kote unakopita, peleka kwa barua pia/ Na uwe na kopi iliyosainiwa na anaeipokea.

Ajabu hii.
 
Ajabu ipi? Inatakiwa muelekeze hivi mimi kutokutambua kama ilipaswa niandikie mkuu wa wilaya barua sikulitambua lakin pia nje ya kulitambua bado napata mazingira magum namna ya kumfikia na kumkabidhi barua yake
 
Hiyo kopi inasainiwa na nani na barua inapita wapi na wapi hebu nifafanulie niandike maana ni zaidi ya mateso kwa vijana mimi sio bodaboda japokuwa mara nyingi ninatumia usafiri wa pikipiki kwa shughuli zangu na hizi adha wenyeji wa dodoma mjini wote hasa wafanyabiashara na wakazi wa majengo wanaijua vzuri sana,mimi hapa nimejitolea kuwapazia sauti kwa kuwa bodaboda ni maisha niliwahi kupitia hata kabla sijawa katika maisha niliyonayo sasa
 
Ajabu ipi? Inatakiwa muelekeze hivi mimi kutokutambua kama ilipaswa niandikie mkuu wa wilaya barua sikulitambua lakin pia nje ya kulitambua bado napata mazingira magum namna ya kumfikia na kumkabidhi barua yake
Pole sana.

Haya anzia kama nilivyokuelekeza. Utaleta mrejesho ulipofikia.
 
Hili kweli liangaliwe polisi Dodoma mjini wanakela sana
Hili la polisi ni Tanzania nzima watu wanalalamika. Ndiyo maana kwengine wanjichukulia sheria mkononi kuwatandika na kuwachomea vituo.


Jeshi la polisi linatakiwa lifanyiwe mabadiliko makubwa sana.
 
Wanakera sana asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…