Sikiliza dogo, mwanamke akikutongoza ukishakubali tu kibao kinageuka! Si kawaida kwa mwanamke kumtongoza mwanaume kwa sababu wana aibu na pia wanaogopa kuonekana changudoa. Inapotokea hivyo ujue huyo mwanamke kakupenda sana kashindwa kuvumilia. Wanawake wengi akikupenda ataonyesha kwa ishara. Ukishindwa kusoma ishara anapotezea au atasubiri siku utakapokuwa interested naye.
Kwa hiyo mwanamke akikutamkia kuwa anakupenda na ukakubali ujue una kazi ya ziada kwa kila hatua itakayofuata. Usitegemee kuwa atarespond haraka kwa kila utakachotaka afanye kwani anataka ujue kuwa hakukutongoza kwa kuwa ni malaya bali kwa kuwa tu kakupenda. Hivyo usitarajie achukue uongozi kwenye mahusiano yenu! Anaweza akawa mpokeaji wa simu na hapigi, hatumi sms mpaka utume wewe, ukitaka kutoka naye ndio kabisa atakusumbua sana! Yaani ni bora uliyemtongoza! Kwa hiyo ukiona hali fulani ya kusuasua usifikiri hakupendi au alikuwa anakutania kuwa na subira endelea kumbembeleza mwishowe mambo yatakaa sawa tu.