opondo
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 526
- 1,321
Habari.
JF imekua ni mwalimu wangu tokea nimeanza kuijua, naelewa humu ndani kuna watu wamepitia mengi sana watanipa ushauri ambao utanijenga Mimi kijana wao.
Imepita mwaka sasa tokea ili swala limetokea nilipokua chuo naombeni ushauri wenu kutokana na experience yenu ambayo mmeshapitia.
Ilikua ni jumamosi nimetoka kanisani nilikua nimelala hostel nikijiandaa kurudi mafundisho ya jioni (Mimi ni msabato), rafiki yangu tunaesoma nae alikuja kuniamsha nimsindikize sehemu flani kwenye maombi ya mchungaji flani (sitamtaja), nilimbishia nikamwambia Mimi sijawai kuhudhuria sehemu yoyote ya maombezi (kutokana na imani yangu). So alinambia nimsindikize tu, nilimwambia Mimi sitahusika na hayo maombezi yao Mimi nikifika nakaa nje, akasema sawa, kwakua alikua ni mshikaji wangu nikaona aina noma Mimi kumpeleka huko.
Kufika huko kanisani tukakaa nyuma nikiendelea kushuhudia nyimbo za mapambio. Kilichonishtusha ni wale wa Mama waliokua wanaongoza mapambio wamevaa suruari zimebana wana "brichi" kichwani (kwa muonekano ni wamama wasiokua na njaa ni wanene na wameng'aa), nikajisemea kimoyo moyo Mungu yupo hapa kweli?
Nikiwa kwenye mawazo mchungaji akatoka kwenye chumba alichokuepo (ofsini ) akaanza kupoint watu means akikushika lazima uende mbele, alifika mpaka tulipokua tumekaa nyuma kabisa akamgusa mshikaji na Mimi akanigusa (ni lazima uende mbele) Baadae ndio nika notice kwamba wageni woote ilikua lazima uende mbele.
Nikaanza kumlaumu jamaa kwanini kanileta huku kwani kuombewa ni lazima?. Mda huo jamaa yangu anatetemeka akanambia Leo tunadondoka mbele za watu aibu ilioje? Nilitamani niondoke nikaona nikiondoka naweza ambiwa nina pepo la kiburi so nikaamua nikaze tu, kufika pale mbele tukaambiwa tuvue viatu hatuwezi kwenda madhabahuni na viatu.
Kwanini nawaomba nyie ushauri?
Kufika mbele Mchungaji akaanza kuomba (tulikua tumepanga mstarii ) so kila anaeguswa na yule Mchungaji alikua anadondoka huku anapiga yoweee...nikajisemea moyoni daah Leo nimepatikana nitadondokaje mbele ya watu aibu ilioje? Nikiomba namba za binti yoyote aliepo mule atanipa kweli? Fedhea gani hiii? .....nikaanza kujilaumu kwanini nisingerudi kanisani kwenye mafundisho..
Ilifika zamu ya rafiki yangu then huyo mchungaji akaanza kusema "wewe kuna mwanamke umempa mimba na unaikataa?" Yule mwenzangu akajibu ndio (Nilikua najua hiyo issue nikawa najisemea Leo Mchungaji atasema siri zangu zote). Mchungaji akaendelea kumuombea huyo rafiki yangu akagoma kudondoka then akanifikia Mimi.
Akaniuliza maswali jina langu nani n.k then akaniuliza ilo jina ni la ukoo au nimepewa? Nikamwambia ni langu la kizungu tu nimepewa. Niliona YouTube yule mchungaji wa Kenya alivyoumbuliwa na aliekua Mwandishi wa KTN Mohammed Ally ambae sasa ni Mp. So Nilikua makini kujibu swali endapo ningesema ni la ukoo angeanza kunambia Mizimu ya ukoo inanifatilia.
Akanambia nasomea nini Chuo? Nikamwambia Bsc in Education (physics)...akanambia naona ulikua unataka kua engineer lakini kuna vitu vimeekufanya umeenda mbali na lengo lako, binafsi nimesoma PCB so wazo la Kua engineer sikua nalo.
Then akanambia nyumbani kwenu kuna utajiri lakini watu wanafanya chokochoko kuwarudisha nyuma. Mzee wangu ni mtu wa dini sana lakini pia uwezo wa kufanya mambo yake ya maendeleo anao, so nikawa najiuliza huyu pastor anazungumzia utajiri gani?...
Mwisho akanambia anavyoona yeye maana ni nabii kwamba nikisomea mambo ya computer nitafanikiwa sana. Alivyoongea hivyo nikawa attention, nilichaguliwa multiple selection nilichanguliwa Computer and software engeneering lakini sikwenda pamoj na Bsc in education, binafsi nimesoma Education tu lakini ni swala ambalo halipo kabisa moyoni mwangu imenifanya nimalize Chuo na GPA ya kawaida maana sikuwai kupenda hata kwenda darasani.
Baada ya hapo aliniombea nikagoma kudondoka akaamua kuniacha tu kwenye kundi ilo kubwaa hatukudondoka Mimi na mwenzangu tu.
SWALI.
Je katika maisha tunayoishi kuna watu wanapitia msoto mkali kwa sababu wamesomea au wanafanya mambo yasiyokua kwenye fani yao au hatma yao? Future au Fate ya mtu tokea anapozaliwa imeandaliwa? Kwamba utapita hapa then uende pengine au ufanye hichi ili ufanikiwe?
Je maisha ni bahati au kupambana? Au ni lazima nikasomee computer kama alivyosema huyo nabii ndio nifanikiwe?....
Nilishakutana na mtu na yeye anasali sana haya makanisa ya kiroho akasema ananiona mimi mbelenii ni mtu mkubwa sana nikabakia kumcheka.. binafsi sina ninachomiliki lakini moyoni mwangu nina spirit kuubwa sana ya kufika mbali nimekua na imagination nyiingi sana kuhusu mafanikio.
ASANTENI.