Habari zenu wanajukwaa, naomba msaada wenu wa mawazo wanajukwaa, nina mwanangu ana miezi minne kwa mda takribani wa wiki mbili anakojoa mkojo wa njano na uchafu wenye rangi km pink,nimeenda hospital wameniambia ni UTI wakanipa amoxlini amemaliza dozi bila mafanikio, kwa wanaojua vizur wanipe chanzo na tiba yake, kuna mfamasia mmoja aliniambia kwa umri wake si rahisi kupata itakuwa kapata infection akiwa tumboni. Je kuna ukweli wowote? Dr mzizimkavu nakusubiria ndugu yangu kazi za watu haziendi