Nisaidieni mwanangu anateseka na ngozi

mataka

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2011
Posts
286
Reaction score
61
Habari zenu wadau, nina mtoto mwenye umri wa miezi 5, alizaliwa dar, baada ya mwezi na nusu akahamia kondoa ndo tunakoishi mpaka leo, baada ya mwezi mmoja ngozi ya mgongoni ikaanza kukakamaa na kutoka. Tukampeleka hosptal wakampa crotimazole cream haikumsaidia, baada ya mda tukaenda tena tukapewa gentalene, nayo haijasaidia,tusaidieni ila haonyeshi kama anaumia. Ila tulipofika tukamwanzishia maziwa ya lactogen kwa kuwa mama yake ni mfanyakazi na ndo hayo anayatumia hadi leo, je hili litakuwa tatizo gani na tutumie tiba gani' au wapi tutapata tiba nzuri?
 
Niliwahi kutibiwa na Dr. Mboneko hapa kwa kairuki sijui bado yupo? maana ni kitambo sana
 
maelezo yako hajitoshelezi sana, ila inabd umwone daktari mtaalamu wa ngozi DERMATOLOGIST, kwa Dar sehemu rahisi itakuwa Muhimbili, au Regency kama utamudu. Kama utaihitaji majina ya hao DERMATOLOGIST in Dar sema.
 
Dr mboneko unaweza pia kumpata kwy clinic yake maeneo ya tank bovu! Siku za kazi ni kuanzia saa 10 jioni, wkend muda wowote
 
maelezo yako hajitoshelezi sana, ila inabd umwone daktari mtaalamu wa ngozi DERMATOLOGIST, kwa Dar sehemu rahisi itakuwa Muhimbili, au Regency kama utamudu. Kama utaihitaji majina ya hao DERMATOLOGIST in Dar sema.

nisaidie ndugu yangu nina mpango wa kumleta dar muda si mrefu
 
mataka, Kuna specialist wa ngozi anapatikana karibia na Muhimbili hospital. ule mtaa wenye supermarket iliyopo bara bara ya umoja wa mataifa karibia na msikiti wa Tambaza.
kama unatokea faya, unakata kushoto(ile suparmarket inakuwa mkono wa kulia) ni ile kona ambayo madaladala ya muhimbili yanapokatia, mita chache baada ya kona upande wa kushoto utaona bango.
Jina la kriniki yake nimesahau.
 
mzizimkavu anajua dawa nyingi mimi zimenisaidia sana ngoja aje akupe darasa
Mkuu Nyasigwa kwa tendo la huyu Mkuu.@mataka Mke wake kumuachisha Mtoto wao Maziwa ya mama mimi pia halikunifurahisha itabidi waende hospitali kutibiwa mimi sitoweza kutoa ushauri wowote ule nimekasirika sana kwanini mtoto wa miezi 5 umuachishe maziwa eti kwa sababu Mama yake amepata kazi yaani kazi ni bora kuliko mtoto wako? Ahhh.😡
 
Last edited by a moderator:
Mpake Aloe vera gel. kuna za special, forever living product or house of health or GNLD, au tafuta kabisa natural shubiri, hiyo ninzuri zaidi. it works magic.
 

asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…