Habari zenu wadau, nina mtoto mwenye umri wa miezi 5, alizaliwa dar, baada ya mwezi na nusu akahamia kondoa ndo tunakoishi mpaka leo, baada ya mwezi mmoja ngozi ya mgongoni ikaanza kukakamaa na kutoka. Tukampeleka hosptal wakampa crotimazole cream haikumsaidia, baada ya mda tukaenda tena tukapewa gentalene, nayo haijasaidia,tusaidieni ila haonyeshi kama anaumia. Ila tulipofika tukamwanzishia maziwa ya lactogen kwa kuwa mama yake ni mfanyakazi na ndo hayo anayatumia hadi leo, je hili litakuwa tatizo gani na tutumie tiba gani' au wapi tutapata tiba nzuri?