Pole sana. Kama walivyoshauri wengine, mpeleke kwa kwa dokta wa watoto. Kwa kuongezea, usikose kumwambia dokta kuhusu matibabu aliyopata na alipata lini. Ni vizuri ikiwa utaonyesha vyeti vyake kama unavyo, ili kuthibitisha unachosema. Kwa matibabu ya mtoto, mimi niko tayari kuonekana mjinga ili nisifanye kosa isije ikanigharimu. Afya ya mtoto naiweka mbele.
Usisahau kumwomba Mungu kwa ajili ya afya ya binti yako (ninaamini hivyo). Kila la heri mkuu.