Nisaidieni umuhimu wa Katiba mpya kwa CCM na wananchi wasio na itikadi ya kisiasa

Nisaidieni umuhimu wa Katiba mpya kwa CCM na wananchi wasio na itikadi ya kisiasa

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
Natamani niwe na mzuka na katiba mpya ila ari haipo kabisa na ninaona wanaotaka katiba mpya wengi ni wapinzani. Je, hitaji hili ni la kisiasa na si haki kama inavyotangazwa?

Kwanini wanaCCM hawana mzuka na katiba mpya? Kwanini wananchi tusio na vyama hatuna maoni juu ya katiba mpya?

Katiba msingi wake wa kwanza ni mwananchi wa nchi husika bila kujali itikadi yake, je hii ya sasa inamkwamisha vipi mtanzania (awe mpinzani au CCM) kufanya mambo yake na ina tatizo gani hata wapinzani hawaitaki?

Kwanini tusifanyie marekebisho sheria mbovu za nchi, tutunge sheria mpya mpya bila kufanya katiba mpya itakayotugharimu hela nyingi zaidi?

Katiba iliyopo iliundwa na watanzania wote waliokuwepo wakati huo, wote tulikua pamoja, ambao ni wapinzani leo nao walikuwepo kwenye kuunda katiba iliyopo wakiwa pamoja na CCM.

Nisaidieni na sheria kandamizi zilizopo sasa ambazo haziwezi kuondolewa mpaka tuwe na katiba mpya.

Nataka kupata mzuka na katiba mpya wakuu, nipeni elimu.
 
Waziri asiwe mbunge, kwasababu mbunge akiteuliwa kuwa waziri wananchi wa jimbo husika wanakosa mtu wa kuwawakilisha bungeni.

Wakuu wa mikoa/ wakuu wa wilaya watoke ndani ya eneo husika.

Kitendo cha kumtoa mtu lindi akawe mkuu wa mkoa kigoma hili haliko sawa kwasababu kiongozi huyu hawezi kuwa na uchungu kwenye kutatua kero za wana kigoma kwa vile kule yeye ni mpita njia.

Mkuu yapo mengi sana sema mimi sio mzuri kwenye kuandika acha niishie hapa.
 
Huku kwetu mbunge akiwa waziri ndo tunafurahi inawezekana hatuelewani bado. Ila haya yote si yanaweza kufanyika bila katiba mpya?
 
Waziri asiwe mbunge, kwasababu mbunge akiteuliwa kuwa waziri wananchi wa jimbo husika wanakosa mtu wa kuwawakilisha bungeni.

Wakuu wa mikoa/ wakuu wa wilaya watoke ndani ya eneo husika.
Kitendo cha kumtoa mtu lindi akawe mkuu wa mkoa kigoma hili haliko sawa kwasababu kiongozi huyu hawezi kuwa na uchungu kwenye kutatua kero za wana kigoma kwa vile kule yeye ni mpita njia.

Mkuu yapo mengi sana sema mimi sio mzuri kwenye kuandika acha niishie hapa.
Oh God. Kwa hiyo kumbe kuna watu hapa nchini ambao wanaonaga kwamba katiba ya nchi ni kwa vyama vya siasa tu? Oh God.
 
Oh God. Kwa hiyo kumbe kuna watu hapa nchini ambao wanaonaga kwamba katiba ya nchi ni kwa vyama vya siasa tu? Oh God.
Hiyo katiba mpya mpaka sasa ni ya upande kisiasa tu. Asasi za kiraia hazijajiubga na kutaka iwepo
 
huku kwetu mbunge akiwa waziri ndo tunafurahi inawezekana hatuelewani bado. Ila haya yote si yanaweza kufanyika bila katiba mpya?
Hii katiba imeshafanyiwa mabadiliko tofauti tofauti zaidi ya mara kumi hadi leo hali inayopelekea saizi kuwepo kwa haja ya katiba mpya.

Mfano una tshart yako mzuri ila kutokana na uchakavu umeshaweka vilaka 8 vipi ikichanika tena hiyo nguo utaendelea kuweka vilaka zaidi au utajipinda ili ununue mpya?
 
hiyo katiba mpya mpaka sasa ni ya upande kisiasa tu. Asasi za kiraia hazijajiubga na kutaka iwepo
Kila kundi linaangalia athari zilizopo kwa upande wao, kwa wana siasa katiba hii inawagusa sana kwenye shughuli zao za kisiasa hasa kwenye issue mzima ya uchaguzi.

Kwasababu kwa katiba ya sasa ni sawa simba na yanga waingie uwanjani halafu refa awe manala unadhani mechi hiyo yanga wanashindaje?
 
Oh God. Kwa hiyo kumbe kuna watu hapa nchini ambao wanaonaga kwamba katiba ya nchi ni kwa vyama vya siasa tu? Oh God.
Yeah, wapo mkuu ila hili halipo kwa bahati mbaya ni vile tu kwasababu tumenyimwa elimu.
 
Kama katiba ya sasa inavunjwa ni vipi katiba mpya itaheshimiwa?

Katiba mpya ni solution inayohubiriwa as though ni mujarabu wa changamoto zote ila kiuhalisia haipo hivyo.
 
hiyo katiba mpya mpaka sasa ni ya upande kisiasa tu. Asasi za kiraia hazijajiubga na kutaka iwepo
Kwa hiyo hata wewe ni wale wale, unachokielewa nii kwamba katiba ni kwa asasi na vyama tu?

Adui wa maendeleo ni ujinga, umaskini na maradhi: (Kwa sauti ya mwalimu Nyerere). Tanzania bado tunayo safari ndefu.
 
Kwa lugha nyingine mkakati yakini! Maaaaweeee! Twafwaaa!
Mambo rahisi haya, haihusiani na elimu. Wanaoomba katiba mpya ni wapinzani, sababu za kuomba ni ili iwe rahisi kwao kuingia madarakani. Ukisema katiba mpya itasaidia kulinda rasilimali zetu bila kufafanua unakua muongo kwasababu sasa hivi kuna sheria kali zinazolinda rasilimali zetu na bado zinakiukwa. Natamani niambiwe umuhimu wa katiba mpya kwa wananchi kiujumla, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini na wasio na dini.
 
Kama katiba ya sasa inavunjwa ni vipi katiba mpya itaheshimiwa?

Katiba mpya ni solution inayohubiriwa as though ni mujarabu wa changamoto zote ila kiuhalisia haipo hivyo.
Wanataka katiba iwasaidie kupata uongozi. Hakuna anaetaja faida kwa wananchi kiujumla
 
Back
Top Bottom