Kapepo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 1,066
- 1,194
Habari wanajamvi nimekuwa nikisumbuliwa na kuwashwa sehemu za siri takribani miaka saba sasa nimehangaika kutumia madawa mengi ya hospital bila mafanikio, imefika kipindi kwenye koo kumekuwa kunawasha kwenye ulimi Kuna utando mweupe pamoja na na kidonda kwa mbali lakin hakiumi shingo yangu imekaza misuli, nasikia ganzi kwenye taya sina raha kwakweli naombeni USHAURI nini nifanye kujikwamua kwenye janga hili hospital zote nilizojarib kwenda wao wamekuwa wakinipatia dawa tu za kumeza na kupaka bila kuchukua vipimo, naombeni msaada wakuu nateseka kuna kipindi mdomoni kwenye lips nasikia kama nimepaka pilipili ni hayo tu wakuu.