Nisaidieni wadau: Pampas zimemtoa vipele mwanangu, nitumie dawa gani?

Nisaidieni wadau: Pampas zimemtoa vipele mwanangu, nitumie dawa gani?

Mrs. Rama

Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
7
Reaction score
0
Habari za kazi,
naomba ushauri wenu juu la tatizo alilonalo mwanangu. nilikuwa namvalisha pampers lakini sasa zieanza kumtoa vipele. nimeacha kumvalisha pampers kw sasa, ni dawa gani ambayo naweza kutumia ili vipele vile vikauke!!!!
 
Pampers gani umetumia? Nunua mafuta ya mgando Vaseline mpake kwenye hivyo vipele atapona. Akiendelea mpeleke hospital.
 
Kuna watu wanachanganya sana hizi diapers za watoto,wengi wanaziita Pampers wakati pampers ni aina mojawapo ya diapers.
 
Habari za kazi,
naomba ushauri wenu juu la tatizo alilonalo mwanangu. nilikuwa namvalisha pampers lakini sasa zieanza kumtoa vipele. nimeacha kumvalisha pampers kw sasa, ni dawa gani ambayo naweza kutumia ili vipele vile vikauke!!!!

Diapers sio nzuri sana kuwavalisha watoto,zinaleta UTI na vipele kwa baadhi ya watoto,cha msingi mnunulie nepi zile za kufunga na pini ndio uwe unamvalisha kwa sana.
 
Diapers sio nzuri sana kuwavalisha watoto,zinaleta UTI na vipele kwa baadhi ya watoto,cha msingi mnunulie nepi zile za kufunga na pini ndio uwe unamvalisha kwa sana.

Ni kweli,usimwache na nguo iliyolowana,mtoto kwa siku anabadilishwa nepi sio chini ya mara 6.kama ni pungufu nenda kituo cha afya
 
Habari za kazi,
naomba ushauri wenu juu la tatizo alilonalo mwanangu. nilikuwa namvalisha pampers lakini sasa zieanza kumtoa vipele. nimeacha kumvalisha pampers kw sasa, ni dawa gani ambayo naweza kutumia ili vipele vile vikauke!!!!

Nilitumia hii kwa mwanangu ilimfaa sana
 
Attachments

  • 1423496879535.jpg
    1423496879535.jpg
    55.1 KB · Views: 796
wavalisheni nepi watoto wawapo nyumbani, na hizo pampers mnapotoka mbali na nyumbani tena sio kwa muda mrefu, hizo zina joto + bakteria, wazungu wameshatuharibia mama zetu.
 
asanteni ndugu zangu, mwanangu kwa sasa anavaa nepi, na vile vipele vyote vimeisha sema vimeacha weupe weupe km makovu and i hope nayo yataisha soon.....
 
Habari za kazi,
naomba ushauri wenu juu la tatizo alilonalo mwanangu. nilikuwa namvalisha pampers lakini sasa zieanza kumtoa vipele. nimeacha kumvalisha pampers kw sasa, ni dawa gani ambayo naweza kutumia ili vipele vile vikauke!!!!

Maisha ya kucopy na kupaste ndio faida zake.
 
wavalisheni nepi watoto wawapo nyumbani, na hizo pampers mnapotoka mbali na nyumbani tena sio kwa muda mrefu, hizo zina joto + bakteria, wazungu wameshatuharibia mama zetu.

Ni kweli wametuharibu ila na sisi tunapenda geza unakuta mtoto kavalishwa diaper moja from asubuhi mpaka jioni unadhani huyo mtoto vipele,UTI N.K hazitampata mtoto kweli??? wakati hao wazungu mtoto akivalishwa diaper akikojoa tu kidogo inatolewa sisi hatuwezi hivyo? na ni bora kumvalisha mtoto nepi..
 
Mmbadilishie aina ya diaper unayomvalisha , kuna nyingi ni cheap qualities ambazo sio friendly kwa baadhi ya watoto zinareact na ngozi zao, usilazimishe aina hiyohiyo..
 
Point SIO kuiga diaper imetengenezwa na material YA cotton ili kunyonya mkojo na kumwacha mkavu ,sasa nepi akishakojolea kunakuaachwa ukavu hapo,pili WENYEWE nepi inakuwa ngumu mtoto akikojolea ️kutokwa Kwenye nguo Ni rahisi na kwao wana winter ️sasa mtoto sindio ataumwa zaidi diaper inatakiwa mtoto abadilishwe kila baada YA 2-3hrs iwapo hajanyea ️sasa wabongo mnabadili baada YA 8hrs ukiuliza maisha magumu ,️sasa si umveshe nepi ambayo unauwezo wa kumbadili kila 2hrs😒😒😒,na usafi wa nepi MUHIMU sana kuuwa bacteria wote mwisho wa siku,unakuta nepi YA mtoto imekuwa green sio white tena ️mie Naona diaper ukipata original ni best💯💯💯
 
Diaperz ni nzuri ila kwa hali ya hewa ya dar es salaam cyo vizuri kumvalisha masaa 24.
Me mwanangu mara nying mchana mamaake huwa hamvalishi ni ucku tukilala na asubuh tu.
Pia ucku huwa tunambadilisha angalau mara mbili.
Ingawa wataalam walitushaur ni bora kumvalisha mchana ucku akalala bila diaper
 
Ninge kusihi pia kwa kumponesha haraka mtafute mtu yoyote agent wa forever living products.wana products nzuri sana hata zakutibu mapele yanayotokana na pamperz,ni pm mrz rama nikufafanulie pitia watsap kwa uzuri na picha na nikutumie waliotumia nakupona kabisa,ama tafuta ma-agent wa FlP
 
tumia mafuta ya mgando mazito ya watoto pia nakushauri tumie New Sleep diaper ni nzur sana...
 
Zinc cream/ointment ni nzuri sana kwa watoto wanaosumbuliwa na upele unaosababishwa na daipers,inauzwa pharmacy na ni maluum kwa kutumika eneo hilo!Jaribu pia kumuacha apate hewa akivua pampers na ukishampaka hio zinc cream yaani mvalishe tu chupi ya kawaida au badili aina ya daiper unayotumia!na usimuache na daiper muda mrefu!
 
Pole sana kwa hilo tatizo la mwanao,ushauri wangu kwako na kwa wenzako muache kutumia hizo pampers,ni vema zaidi ukatumia nepi au hata vitambaa vya khanga na vitenge kumfunga mtoto wako,na kikubwa zaidi kama nyumba ni yako mvalishe mtoto chupi tu pindi awapo nyumbani na umpe uhuru wa kukojoa hata kunya pindi apatapo haja,hii husaidia kutokomeza vibamia kwa watoto wa kiume,cha msingi zaidi nashauri hata akina mama na akina dada waache mara moja kutumia pedi na warudi kwenye kuweka vipande vya kangha,vitenge pindi wawapo kwenye hedhi.Ninauzoefu na haya mambo nimeshuhudia kesi nyingi za madada,wamama kujikuna sehemu zao nyeti au kuwa nyeusi tii,kisa kutumia hizo pedi,namalizia kwa kusema huu ni ushauri tu mwenye macho na masikio ana uhuru wa kuuchukua au kuuacha!!!

Back
Top Bottom