mkuu
pole sana. kweli dunia ina mambo??
Nakushauri umsamehe, umepoteza vingi juu yake, na zaidi anakujali sana tu. Inawezekana alipata mtu wa kumdanganya, ndio maana akafanya jambo la kijinga.
Mpe nafasi nyingine. hakuna binadamu aliye sawa (perfect). wengine wanayafanya haya wakiwa ndani ya ndoa.. Lakini give her a chance..
Ukimsamehe toka moyoni, Mungu ni mwema, atarekebisha uhusiano wenu..Kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana, ukitaka kuchukua hatua kwa kila tukio, utakufa mapema.
Wanadamu tuko hoi siku zote, pamoja na Mungu kutuma hata Mwanaye, lakini mambo bado sio mazuri kote misikitini na makanisani. MSAMEHE.
Siafiki wala kuunga mkono ujinga wake huyo dada, isipokuwa wanadamu tunateleza sana, kama sio leo basi ni kesho. She is yours, unamjua vizuri sana na yeye vivyo.. Nakuhakikishia kuwa atakuwa na heshima kuliko wakati mwingine wowote..Mshirikishe Mungu katika uamuzi wake.
thanks