Nisaidieni

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
461
Reaction score
392
Kila toleo jipya la simu anataka nami sina noma namnunulia na juzi juzi kaja anataka laptop ili amalizie kazi zake za chuo kwa muda muafaka nami niaona ni jambo jema nikamnunulia.

Wiki chache zilizopita nikasafiri na kwenda Mbeya ili niweze kumsalimia mpenzi wangu kwa suprize na kwa kuwa mie nina rafiki yangu aishie huko na huwa nafahamu anakoishi nikaenda moja kwa moja kwa rafki bila naye kumwambia.

Kufika geto kwa jamaa naona ile laptop iko pale na jamaa ukitani kapamba picha za mpenzi wangu na kama haitoshi simu anayoitumia ni ile mpenzi aliyosema amaeibiwa kwani nakumbuka kava lake niliweka lenye picha ya mchezaji wa MAN U.

Nkiwa nazidi kupepesa macho naona na baadhi ya nguo za yeye ziko pale.Sikuongea kitu na kwenda hotelini na siku ya pili kusafiri kurudi dar, Hapa nimechanganyikiwa na sijui nini nifanyeje na wao wamekuwa wakinipigia simu kusema yaishe.

Naombeni msaada wa nini cha kufanya marafiki.
 
Mpotezee tu... Tho it pain.
We wampenda ila yeye anampenda mwingine. Ndo mana kakutenda ivyo
 
Rafiki yako ndiyo adui yako kaa ukajua....MR.achana nao watakukwamisha kwenye utafutaji wako,ila ukisalimiwa nao waitikie kwa amani ili wao waonekane wajinga kwa kukufanyia uchafu..pole mzee ndo changamoto za mapenzi:israel:
 
Ulifanya vizuri kwa suprise la safari,maana mpenziwe alikuwa analengo la kukukomoa kiuchumi......
 
haaaa inaonekana jamaa ww ni mpole ndo mana ulivyowakuta wakakwambia yaishe sasa maana ya yaishe wanakupa vitu vyako halafu wanaendelea na mambo yao au
 
Mh...maisha haya, kuna rafiki yangu yeye anasema msichana yeyote anae kuwa nae akifika chuo tu anamuacha, nadhani alikuwa anaogopa mambo kama haya, mie binafsi nnasema kama ni demu wangu akifika chuo na mimba anayo ili akileta ujinga ajue anajikomoa mwenyewe.

Pole ndugu, hao ndio wasichana wa chuo, ni balaa tupu.
 
Kweli umevurugwa hadi umekuja kupost huku! Lakini huku kwetu kila kitu wanajua utani tu!
 

wewe ni ATM inayoishi......
 
kama alphonce,, waambie wakupe v2 vyako usepe ukatafute mwngne wakumpa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…