Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
Na Alli Mayai
Tangu sakata la Manara na Simba lianze sikuandika makala yoyote juu ya sakata hilo. Ulianza kutembea sauti ya Manara akimtukana CEO wa Simba, Barbara Gonzalez, baadae maelezo meengi na post nyingi za Manara zikafuata kwenye account zake za mitandao ya kijamii, baadae bodi ya wakurugenzi ikamtangaza Ezekiel Kamwaga kuwa kaimu mkuu wa idara ya habari (automatically Manara akawa ameondolewa) na majuzi Manara kaitisha mkutano wa wanahabari ambapo alitema "nyongo".
Sasa nijibu haya maswali:
1. Manara hakufanya mazuri Simba?
Jibu ni hapana. Manara amekuwa mtu muhimu Simba kwa kipindi alichokuwepo takribani miaka sita. Kwa nafasi yake alijitahidi kiasi chake.
2.Simba inaweza kufanya vizuri bila Manara?
Jibu ni ndiyo. Simba haijaanza kufanya vizuri chini ya uafisa habari wa Manara, imechukua ubingwa wa kagame mara 6 bila Manara, imefika fainali 1993 michuano ya CAF bila Manara, imefika makundi 2003 bila Manara, imedominate Soka la ndani kwa nyakati tofautitofauti bila Manara. Na itaendelea kufanya vizuri bila Manara imladi kama uongozi unapita kwenye njia sahihi za uendeshaji timu, usajili mzuri, bonus kwa wachezaji na mpangilio mzuri. Kuondoka kwa Manara hakuwezi kuirudisha nyuma Simba.
3. Manara na Simba nani kanufaika zaidi kwa mwenzie?
Jibu ni Manara: Kabla Manara hajaja Simba ni wachache walimfaham wakati akiwa kwenye siasa za CCM kule Dar es salaam, akiwa gazeti la Uhuru na akiwa mchambuzi wa mpira kwenye TV, alifahamika kwa wachache. Kuja kwake Simba ametengeneza wigo mpana wa kufahamika kwa watu wengi ambao hawakumjua ghafla.
Akapata mashabiki Wengi kwenye account zake za mitandao ya kijamii, akapata matangazo ya biashara Kutokana na umaarufu aloupata kupitia Simba. Simba nayo kwa kiasi chake imefaidika kuwa na Manara kwa hamasa zake. Ila yote kwa yote Manara kanufaika zaidi.
4. Ni sahihi SIMBA kumtema Manara na Barbara kubaki ofisini?
Jibu ni; sahihi. Barbara ni CEO, ni bosi wa watumishi wote pale Simba, ni mtendaji na mfuatiliaji shughuli zoote za klabu na idara zote ikiwemo idara ya habari ya Simba iliyokuwa chini ya Manara. Kama Manara anamfokea bosi wake (CEO, Barbara) maana yake hawawezi tena kufanya kazi pamoja. Je, umuondoe CEO kisa kumbakisha afisa habari? Jibu ni haiwezekani. Hivyo ni sahihi kumwondoa Manara akabaki CEO.
5. Simba inaweza kupoteza mashabiki kisa kumfukuza Manara?
Nacheka kwanza [emoji1787][emoji1787] hafu nasema "sidhani japo inawezekana". Kwenye mpira huku Kuna watu Wana akili timamu, Kuna wasio timamu, Kuna fuata upepo, kuna wanaopenda wachezaji, kuna wanaopenda timu, na kuna wachache wanaopenda viongozi tu (hao ndo wanaweza kuhama kwasababu ya Manara) japo nasisitiza kuwa sidhani. Yaani shabiki wa Simba ahame kisa Manara? Hafu ahamie Azam, Lipuli, Mwadui au Yanga? Sidhani japo yawezekana.
6. Je, Manara yuko sahihi kuongea aliyoongea juu ya Simba?
Manara hayuko sahihi hata kidogo, yawezekana aliyosema baadhi yakawa sahihi lakini huwezi kwenda kuanika hayo kwenye media. Kulinda "image" yako na ya taasisi uliyotoka busara huwa ni kukaa kimya. Unaweza ukaongea vitu sahihi kwa wakati usio sahihi ukajishusha Mwenyewe.
Baada ya majibu hayo, nyongeza ni hii;[emoji116][emoji116]
Sauti ya Manara iliyosambaa mitandaoni inasikika yeye pekee akigomba na kutukana. Hakuna anayemjibu. Maana yake ile ilikuwa 'WhatsApp voice call' na mule anasikika akisema ".. na hii naisambaza kwa viongozi wote..." Maana yake yeye mwenyewe ndo chanzo Cha kusambaza sauti ile mitandaoni ingawa yeye huyohuyo anasema Barbara aliisambaza, anasahau kama amesema ataisambaza kwa viongozi wote.
Manara anasema Mohammed Dewji anamuonya juu ya kuwa maarufu kuliko yeye [emoji1787]!! Mmh, hapa napo pana shida. Yaani Mo aliliye umaarufu? Hadi amuonye Manara?? Tajiri kijana namba moja Afrika, Tajiri namba Moja Tanzania, mfanya biashara mkubwa, mshauri wa masuala ya uchumi wa rais wa South Africa, Cyril Ramaphosa, mtu aliyewahi kuwa Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10, mtu aliyewahi kuwa mjumbe wa NEC (CCM) leo hii 2020 aliliye umaarufu na Manara?? Za kuambiwa changanya na zako [emoji625][emoji419].
Manara anasema Barbara ndo chanzo cha watu wengi kufukuzwa pale Simba na hapohapo anasema Senzo alipokuja aliambiwa amfukuze, kumbuka Kabla ya Senzo CEO wa kwanza Simba ni Crisentus John Magori. Sasa wakati Senzo anakuja Barbara hakuwa na nguvu yoyote kwenye bodi ya wakurugenzi wa Simba na mwenyekiti alikuwa "Try Again" sasa kama Senzo aliambiwa amfukuze kazi maana yake bodi tangu awali ilikuwa haimkubali? Na ilishindikana nini kufukuzwa? Yaani Senzo aliivimbia bodi ya Wakurugenzi wa Simba akashindwa kumfukuza Manara? Za kuambiwa changanya na zako.
Manara anasema analipwa laki 7 (700,000/= per month) fine, ila anakili kupewa mkataba wa million 3 kama si nne wenye masharti ya kutotangaza bidhaa za GSM na Bakheresa. Sasa ni mkataba gani wa kazi usiyo na masharti?
Manara anasema alikuwa hakatiwi tiketi kwenda mechi za mikoani, sawa. Kwani alikuwa na umuhimu mkubwa kuhudhuria mechi za Simba za mikoani? Kama ndiyo, kwanini mechi nyingi za Simba za Dar es Salaam alikuwa haji uwanjani? Umuhimu wake ulikuwa mechi za mikoani kuliko mechi za Dar es salaam? Jibu hapana, ila ULAJI, mikoani alikuwa ana fursa ya kuchangisha mashabiki na kutokomea na hela.
Yote kwa yote Manara anaweza kuwa na hoja sahihi ila si yoote aliyosema. Na aache kupenda kutafuta huruma ya mashabiki. Ajifunze kubadilika kulingana na nyakati. Zama za ujanjaujanja zimepita. Atambue mashabiki wanataka kuona Mpira ukichezwa na timu yao ikifanya vyema. Sasa kunyamaza ni njia sahihi kwake haijalishi anaongea ukweli au uongo kuchafua viongozi na kutafuta huruma ya mashabiki.
Wasalaam,
Ali Mayai
Safarini Uyu