mkamanga original
JF-Expert Member
- Jan 21, 2015
- 637
- 663
Napingana sana na wana harakati na waumini wanao dai sasa nchi inahitaji katiba mpya ili iweze kwenda mbele.Mimi napingana nao kwa sababu kuu zifuatazo
1. Kwa sasa kudai uandaaji wa katiba mpya ni kupoteza fedha na muda kwa sababu sisi kama nchi bado hatuna uwezo wa kuisimamia hiyo katiba mpya. Sisi wananchi tulio wengi hatujafikia kuwa na uwezo wa kusimamia kile kilichopo ndani ya katiba, hivyo hata ikatengenezwa haitakuwa na manufaa kwa wakati huu. Ninamaanisha hatuna uwezo wa kumchukulia hatua kiongozi yeyote atakayeonekana kukanyaga hiyo katiba .Mfano mdogo ni utawala uliopita tumeona ukanyagaji mkubwa wa katiba kuanzia kwa Rais hadi kwa akina Sabaya, lakini wananchi hatukuthubutu hata kunyoosha vidole, ndio maana nasema kizazi hiki bado sana . unaweza ukaandaa katiba Leo na kuweka misingi imara lakini baada ya miaka 4 anatokea mpumbavu mwingine anaendesha nchi kama familia yake , kizazi hiki tujiulize wote kuna mwananchi anayethubutu kuingia mitaani au kumnyooshea kidole unavunja katiba. Kizazi hiki hakija andaliwa katika ujasiri huo. Labda tusubiri kikazi kilichozaliwa miaka ya 2020 na kuendelea
2. Sababu ya pili wasomi wetu ni hopeless kabisa ,wapo kufuata upepo ,na ushaidi wa hili lipo wazi katika utawala wa serikali ya awamu ya 5. Katiba ilikanyagwa katika maeneo mengi lakini hakuna cha wasomi wala wanasheria walio thubutu kupanua ndomo ,kila mtu aliufyata, wachache sana walijitokeza kupiga kelele lakini hawakuungwa mkono na hao tunao wahita na kuwaona wasomi . sasa kwa mantiki hiyo ndio tupate katiba hiyo mpya kuwategemea hao wachache Akina Liisu , haki za binadamu watupiganie? Si kupoteza muda tu. Ni bora tusubiri hadi wasomi wetu watakapokuwa na uwezo wa kujisimamia ndio tuandae hiyo katiba mpya. Wasomi wetu bado hawajakomaa kuweza kusimamia na kuwaongoza wananchi kudai kile kilichopo ndani ya katiba. Wasomi wetu wengi waliopo hawajajengewa ujasiri wa kutosha ,ni waoga, wasaka fursa . Wengine hivi sasa ndio wanaonekana wana ujasiri lakini ukweli ni kwamba nchi hii kwa miaka 5 alikuwa mwanaume mmoja tu wengine wote tulikuwa kama wanawake tu kwenye nyumba ya baba aliyeamini kwamba wote ni watoto tu tulip wajinga tusiojua chochote
Ushauri:
Ni bora tu tuendelee kuweka vitaka katika hii iliyopo hadi tutakapoona sasa wasomi wetu wanajielewa, na wameanza kuamini ka na wananchi. Wasomi tulip nao sasa hawaaminiki hata chembe na wananchi sasa kutokana na yaliuokuwa yanaendelea katika utawala wa awamu ya 5