Niseme Ukweli. Katika kutafuta mchumba humu mitandaoni nlikutana na watu wa ajabu sana

Niseme Ukweli. Katika kutafuta mchumba humu mitandaoni nlikutana na watu wa ajabu sana

Tusichokubali au tusichokielewa ni kwamba tulioko huku JF ndio haohao walioko huko makazini au mitaani kwetu,tofauti ni kwamba hapa hatujuani tu.
Ila nimependa umesema ukweli mchungu wengi humu tunajikuta maslay queen wakati nje ya hapa uhalisia wa maisha yetu unatisha hivyo hivyo kwa wanaume wa humu.
Hapo kwenye elimu ndo penyewe kabisaaa ujuaji mwingiiii na kutaka kuonekana kila mahali wakati ni zero Brain.
Anayekuambia ukweli anakupenda nakuunga mkono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je wewe ni mfanya biashara, una shule, chuo, ama biashara yoyote na umekuwa na shida ya kujitangaza, unabiashara ndogo na haiendi kama unavyotegemea, basi tupo hapa kukusaidia kuwafikia wateja wako wengi kwa wakati mmoja. TANWEB group of proffessional wa I, tunakutengenezea website kwa gharama nafuu sana ya laki moja tu Tsh.100,000/=na utalipia domain name kwa elf 80 mwaka mzima. Na kama hauna elf 80 usihofu, utalipia laki moja 100,000/= utatengenezewa website yako na utapewa subdomain bureeeeee kabisa bila malipo yoyote. Offer hii ni kwa mwezi January na february pekee baada ya hapo tutaendelea na bei zetu kama kawaida. Tupo Musoma mjini na utatupata kwa namba 0782183441 au 0623523538 karibu sana tukuunganishe na wateja wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzo nlikuwa naamini wanawake walioko JF ni big brains, smart ones. Nikajiaminisha kwamba hapa ndo mahali pazuri pa kupatia mchumba.

Sikuwahi kuandika uzi wa kutafuta mchumba, but nimewafuata wale wanaotafuta kwenye PM zao sana. Nikaja kubahatika kumpata mdada mmoja ambaye niliona atanifaa kwani tulikuwa tunaendana kwa % kubwa plus tunatoka mkoa mmoja.

Tulianza mahusiano vizuri kabsa ambayo yalidumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Lakini mateso aliyokuja kunipa sitokaa niyasahau kamwe maishani mwangu. Mateso aliyonipa yule mwanamke yalikuw makubwa mnoo kwani yaligusa kila nyanja ya maisha yangu mpaka kazi yangu. Kwa funzo alilonipa yule mwanamke sidhan km kuna mwanamke atanipa shida tenaa maishan mwangu.

All in all namtakia maisha mema na Mungu ambariki.
Pole....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wa jf nyie ndio hamnaga mirejesho eeh, maana kila siku naona kaka zenu wanavyowanyumbua lakini nyie kimyaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahaa!

Kusema ukweli haya mambo [hizi mada] huwa yana msimu wake.

Leo jamaa kaliamsha dude dhidi ya wachuchu. Majuzi hapa DaJane naye alilianzisha dhidi ya ‘wanaume wa JF’.

Kuna kipindi pia wanaume waliandamwa sana hadi kupewa majina ya ‘Pugi’, mara sijui ‘Bwana Pepsi’, mara sijui nini...n.k.

Ukiwa objective observer utagundua kuwa jinsia zote huwa zinashambuliana shambuliana.

Hivyo, kimsingi hii mada haina jipya. Haya mambo yameshajadiliwa sana huko nyuma, yanaendelea kujadiliwa, na yataendelea kujadiliwa.

Labda kilicho kipya hapa ni mwanzisha mada tu kuwa tofauti. Lakini maudhui ni yale yale.

Na naweza kuweka dau [licha ya umaskini wangu huu] kuwa huu si mwisho wa mada zenye haya maudhui.

Muda si mrefu atakuja mtu mwenye ID ya mdada na ataanzisha mada ya kuwaponda ‘wanaume wa JF’.

Watch this space.....
 
Back
Top Bottom