SoC03 NISHATI MIX-Mashine ya kuzalisha umeme pamoja na gesi kwa kutumia Plastiki na Uchafu unaooza

Stories of Change - 2023 Competition
Really amazing for sure am interested taifa needs people kama ww kwa its prosperity
Thanks , Mimi na wewe ni taifa la kesho ,tushirikiane kutatua matatizo kwenye nchi yetu.
 
 
Kwenye hili ndugu umeliweza usafi ubora nishati🙏
 
It’s very peculiar that you brothers came up with such convincing idea mostly applicable in our daily life, it’s very pleasing and I gladly congratulate to your efforts. Keep it up, I think popular recognition on this project can be of more help, especially by authority. Keep the spirit burning 🙏
 
Thanks for recognition, and views on the project, knowing that only the best is good enough .
 
Yuh Der Best keep it Bruh... We on Der way Support what yuh start creating ✊❤️
I am profoundly grateful . Your appreciation serves as a powerful affirmation of my dedication and encourages me to continue striving for excellence
 
Wow! this is so good congrats 💪
 
Wazoo lako ni zuri kijana, lakini sayansi yake kama hujaichanganya basi ina shida ambazo bado hujazielezea.

Kwanza: Mfumo wa kuchoma na pyrolysis ni kitu kimoja. Kulingana na maelezo yako, umesema mashine inachoma bila kutumia hewa (ambayo ni pyrolysis - kuchoma dutu bila kuwepo kwa oksijeni). Sasa, mfumo gani wa kuchoma utatumika?

Pili: Mchakato wa pyrolysis unafanyika kwa joto lililoinuliwa (nyuzi joto > 500⁰C). Je, utatumia aina gani ya nishati ili kufikia joto hilo bila gharama kubwa?

Tatu: Mchakato wa pyrolysis unazalisha gesi taka mbaya kwa mazingira kama Methane (CH4), kabondaidioksidi (CO2), gesi za NOx, na kadhalika. Hii ni kwa sababu unachoma plastiki ambazo zinajumuisha polymer. Je, umepanga jinsi ya kukusanya gesi hizo ili zisitolewe kwenye mazingira? Unahitaji mfumo thabiti kwa hili.

Nne: Wazo lako lingekuwa bora zaidi kwa taka ambazo haziozi, kwa sababu hizo ndizo zinazosababisha matatizo kwa mazingira. Hata hivyo, taka ambazo zinaoza zinaweza kutumiwa kama mbolea badala ya kuziongezea gharama. Kuchakata plastiki kwa gharama hizo zote, wakati unaweza kuzitumia tena (kuzirecycle) kutengeneza plastiki mpya kwa urahisi...?

Ushauri wangu:

1: Ingependeza zaidi ikiwa ungeambatanisha matokeo ya bidhaa zilizokamilika, gharama ya kuendesha mashine, na kiasi cha nishati unachoweza kutengeneza kutoka kwa kilogramu 10 ya plastiki...

2: Wasiliana na wahandisi wa kemia ili upate ufahamu zaidi na pia upate "material and energy balance" (usalama wa vifaa na nishati).
 
Asante kwa Maoni Mr Charles,sijaweza kuambatanisha taarifa zote kutokana na kiwango Cha maneno yanayotakiwa na waandaaji wa stories of change .Lakini pia kuhusu gesi chafu ,hazitoki ndani ya mashine ,Kuna catalyst pamoja na filters zinazozuia gesi chafu kutoka ndani ya mashine ,kwenye mfumo wa uchujaji . Tunatumia Induction heating principle kwenye kupata joto.,Kwa maelezo zaidi unaweza tembelea kurasa za mitandao ya kijamii na kama upo DSM kwa sasa nakualika kwenye 47th DSM international trade Fair DIFT yanayoanza tarehe 28 mwezi huu mpaka tarehe 13 julai kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ,nitakuwa kwenye banda la UDSM kwa ajili ya maelezo zaidi.Karibu sana.
 
Weka pia video fupi ya namna mashine inavyofanya kazi.
 
Hongera, ni wazo zuri, ila nahisi utapata challenge kidogo kwenye biashara sababu ya, ATTITUDES zetu kama jamii,hatuchukuliaji uchafu kama responsibility yetu, ngumu mtu anayekula ndizi na kutupa au kutupa chupa ya maji iliyotumika hovyo leo aanze kuona umuhimu wa kumanage uchafu kwa kuwa na machine.

Kwenye marketing nahisi ujumuishe content itakayobadilisha mindset zetu, mimi siijui strategy lakini unaweza kwenda direct mfano ''kila mtoto mmoja hufa kila saa kutokana na kilo moja ya uchafu unaoachwa kiholela (ni mfano tu), watu wakianza kuwa conscious na uchafu wataona umuhimu wa kuusimamia vizuri hivyo kununua machine ya kudhibiti uchafu. (Ninahisi tu),
 
Asante kwa Maoni .
Kubusu hizo plastics na organics tunaziprocess wenyewe na kuziweka kwenye blocks (vipande) ,ambapo hizi blocks ndo zitaingizwa kwenye mashine kwa Ajili ya kuiendesha ...mnunuaji haitaji kutafuta uchafu atanunua blocks zilizo tayari .
 
Sawa Ila kama umelenga mtu
Mmoja mmoja, kunahitaji jitihada za zaidi kuwa persuade kutokana na attitudes zetu.

Sijui Km ni wazo la kitoto Ila Ningependa kuona investor mkubwa kama serikali inunue machine zako na kuzisambaza , uingie contract ya kutengenezea Ama kuiuzia serikali lol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…