Nishati Safi ya Kupikia: Je Tunahitaji Zaidi Utashi wa Kisiasa, Political Will, au Mahubiri ya Nishati Safi, Huku Mazingira Bado ni ya Kuni na Mkaa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la leo.
1728817428312.png

Utekelezaji wa hoja ya Nishati safi ya kupikia, unahitaji zaidi utashi wa kisiasa kuliko ahadi za maneno na kuwagawia bure mitungi ya gesi watu masikini wa kutupwa wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambapo hawana uwezo wa kununua gesi hiyo. Madam tuna umeme karibu nchi nzima, utashi huu wa kisiasa ungeanzia kwenye umeme, kitu kilichopo kisha ndio tuje kwenye gesi!

Leo naendelea na sehemu ya pili na ya mwisho ya nishati safi ya kupikia

Watanzania ni wazuri sana kwa mahubiri, preaching, lakini inapokuja kwenye suala la kutekeleza kwa vitendo kile kinachohubiriwa, (practicing what we preach), ni mbingu na nchi.

Kwa sasa, kuna hii single mpya ya Nishati safi ya kupikia, ambayo sterling wake ni Rais Samia Suluhu Hassan, na mkazo umewekwa kwenye gesi ya majumbani na matumizi ya nishati jadidifu.

Wiki iliyopita niliishia kutoa wito, wa hiki kinachofanywa na Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, kuunga mkono juhudi za Rais Samia, kwa kuanza kusambaza gesi ya kupikia, kwenye vituo vyaka zaidi ya 100, vilivyotapakaa nchini kote.

Niliishia kutoa sababu ya ni kwanini Watanzania wengi bado wanakumbatia matumizi ya kuni na mkaa kwa nishati ya kupikia?. Nikajijibu, jibu ni moja tuu, majiko ya gesi ni gharama na gesi, na majiko ya umeme na gharama za umeme ni ghali kuliko mkaa, kuni kwa vijijini ni bure, ughali huu unachangiwa na kodi na tozo mbalimbali, hivyo kama serikali yetu iko serious Watanzania watumie gesi, na ina political will, ifanye yafuatayo….
Leo naendelea na mapendekezo yangu.
1. Pendekezo kuu la kwanza, ni uwepo wa utashi wa kisiasa (political will), wa nia ya dhati ya Watanzania watumie nishati safi ya kupikia ya gesi na umeme badala ya kuni na mkaa. Kwa vile kampeni hii inaongozwa na Rais Samia mwenyewe, tunaweza kusema utashi wa kisiasa upo, lakini jee kuna hatua zozote mahsusi za dhati kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia?.

2. Serikali ifute kodi zote kwenye majiko ya gesi, mitungi ya gesi na gesi yenyewe, na kwenye majiko ya umeme na kushusha gharama za umeme. Kuna ubaya gani serikali ya Mama Samia, ikaondoa kodi zote kwenye ikiwemo VAT kwenye majiko ya gesi, umeme na gesi ya kupikia?. Mbona kwenye computes tumeondoa kodi?. Hawa Watanzania wenzetu elfu 22, wanaokufa kila mwaka kwa matatatizo yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, maisha yao yangeokolewa kwa matumizi ya gesi na umeme.

3. Wanasheria tuna msemo wa “exhaust local remedies” yaani kabla hujatafuta msaada wan je, anza na kile ulichonacho. Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiua nyoka, fimbo ya mkononi ndio uiwayo nyoka, kwenye huu mkakati wa rais Samia wa nishati safi ya kupikia, nishati ya gesi ni fimbo ya mbali, inayohitaji mitungi, na kusafirishwa, lakini kwa sasa zaidi ya asilimia 90% ya nchi yetu, tuna umeme, hivyo fimbo ya kweli ya karibu, ni majiko ya umeme, na sasa kuna majiko banifu ya umeme mdogo, ma rice cooker, na fryers, na pressure cookers. Serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya umeme wa kupikia, kama kwenye computers tumeweza, tunashindwa vipi kwenye majiko ya gesi na umeme?.

4. Serikali itambulishe ruzuku ya majiko ya gesi, umeme na mitungi ya gesi, kama ruzuku kwenye zana za kilimo na pembejeo ikiwemo mbolea. Enzi za Mwalimu, baadhi ya bidhaa muhimu zikiwemo, mbegu, mbole na pembejeo za kilimo, zilifanywa bei nafuu kuliko hata bei halisi kwa kupewa ruzuku ya serikali ili wananchi wamudu gharama. Kuna wakati wa uhaba wa maji, Tanesco ilikuwa inatumia gharama kubwa kuzalisha umeme wa gesi na mafuta na kuuza kwa bei ndogo kama ya umeme wa maji ili kutowabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama

5. Wafadhili mbalimbali wahamasishwe kujitolea kufadhili majiko na mitungi ya gesi kwa wasio na uwezo, wakiwemo TASAF iingize program ya kufadhili majiko, mitungi na ruzuku ya gesi kwa kaya masikini katika program yao ya kunusuru kaya masikini.

6. Tutunge sheria ndogo, by laws, kulazimisha taasisi zote za watu wengi, mashule, vyuo vya kati, vyuo vikuu, na mahoteli ni lazima kutumia ama biogas, ama gesi ili kuokoa mazingira na sheria za ujenzi zijumuishe njia za kesi kama ilivyo kwa mabomba ya maji, umeme na mawasiliano, watu walipe bili za gesi kama maji na umeme.

7. Ziwekwe tozo maalum kwa vibali vya mkaa, na ziwekwe faini kali kwa uharibifu wa misitu kutafuta kuni na uchomaji mkaa bila vibali. Kama Tanesco iliweza kuuza umeme kwa bei ya chini, na enzi za Mwalimu kulitolewa ruzuku kwenye bidhaa muhimu, na enzi za JPM, gharama za kuunganishwa umeme wa REA, zilikuwa ni Shilingi 27,000 tuu, na tumeshuhudia hadi vijumba vya nyasi, vimeunganishwa na umeme, hili linashindikana vipi kwenye gesi?.

8. Tuongeze matumizi ya mkaa wa mawe na mkaa mbadadala , na kuongeza matumizi ya majiko banifu.

9. Wenzetu walioendelea, gesi inasambazwa majumbani kwa mabomba kama maji na umeme, then vijiji vyote vinavyopitiwa na bomba la gesi, visambaziwe gesi majumbani kama ulaya, Tulielezwa itasambazwa hadi majumbani, kama Tanesco wameweza kusambaza umeme kote, maji pia yamesambazwa kote, TTCL inasambaza mkongo wa taifa hadi majumbani, kunashindikana nini kusambaza gesi hadi majumbani watu wakalipa bili za gesi kama ulaya?.

Mungu Mbariki Rais Samia aliweze hili la Nishati safi ya kupikia
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la leo.
View attachment 3123480

Bado jamii yetu inategemea mno kuni na mkaa kupata nishati....ni vyema tuangalia namna tunaweza kupungiza matumizi makubwa ya kuni na mkaa kwa kupata majiko yenye kutumia mkaa au kuni chache ila yanahifadhi joto kwa wingi.....huku tukiendelea taratibu kunadi nishati za umeme na gesi ikiwezekana taasisi zote za Umma zianze matumizi ya nishati safi kwanza kabla ya raia.

Huu ni mchakato unahitaji muda na gharama kuufanikisha.
 
Kwamba tuondoe Kodi kwenye Gesi na kuweka Ruzuku ili watu wanunue majiko ya gesi na kujaza gesi ? To what end ?

Hili jambo rahisi sana hakuna haja ya kugusa gusa hapa na pale ni kwamba wamalize Bwawa overheads obvious zitapungua na bei ya umeme ishuke hata hadi 20/=.., after all mpaka dakika hii vijijini umeme unit moja ni 100/= na mtu akinunua mtungi wa gesi mdogo kujaza ni almost 300/=..., sasa kwanini ukweli huu hausemwi ?!!!

Kuliko kuendelea kupiga kampeni ya kuuza gesi na kuwachanganya wananchi hio promotion za gesi tuwaachie kina Oryx na Taifa gesi..., sababu wana stake ya kupata faida ila ukweli ni kwamba kwa kumsaidia mwananchi ki ukweli ni UMEME pekee ndio jibu kwa Mwananchi

Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la leo.
View attachment 3123480
Utekelezaji wa hoja ya Nishati safi ya kupikia, unahitaji zaidi utashi wa kisiasa kuliko ahadi za maneno na kuwagawia bure mitungi ya gesi watu masikini wa kutupwa wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambapo hawana uwezo wa kununua gesi hiyo. Madam tuna umeme karibu nchi nzima, utashi huu wa kisiasa ungeanzia kwenye umeme, kitu kilichopo kisha ndio tuje kwenye gesi!

Leo naendelea na sehemu ya pili na ya mwisho ya nishati safi ya kupikia

Watanzania ni wazuri sana kwa mahubiri, preaching, lakini inapokuja kwenye suala la kutekeleza kwa vitendo kile kinachohubiriwa, (practicing what we preach), ni mbingu na nchi.

Kwa sasa, kuna hii single mpya ya Nishati safi ya kupikia, ambayo sterling wake ni Rais Samia Suluhu Hassan, na mkazo umewekwa kwenye gesi ya majumbani na matumizi ya nishati jadidifu.

Wiki iliyopita niliishia kutoa wito, wa hiki kinachofanywa na Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, kuunga mkono juhudi za Rais Samia, kwa kuanza kusambaza gesi ya kupikia, kwenye vituo vyaka zaidi ya 100, vilivyotapakaa nchini kote.

Niliishia kutoa sababu ya ni kwanini Watanzania wengi bado wanakumbatia matumizi ya kuni na mkaa kwa nishati ya kupikia?. Nikajijibu, jibu ni moja tuu, majiko ya gesi ni gharama na gesi, na majiko ya umeme na gharama za umeme ni ghali kuliko mkaa, kuni kwa vijijini ni bure, ughali huu unachangiwa na kodi na tozo mbalimbali, hivyo kama serikali yetu iko serious Watanzania watumie gesi, na ina political will, ifanye yafuatayo….
Leo naendelea na mapendekezo yangu.
1. Pendekezo kuu la kwanza, ni uwepo wa utashi wa kisiasa (political will), wa nia ya dhati ya Watanzania watumie nishati safi ya kupikia ya gesi na umeme badala ya kuni na mkaa. Kwa vile kampeni hii inaongozwa na Rais Samia mwenyewe, tunaweza kusema utashi wa kisiasa upo, lakini jee kuna hatua zozote mahsusi za dhati kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia?.

2. Serikali ifute kodi zote kwenye majiko ya gesi, mitungi ya gesi na gesi yenyewe, na kwenye majiko ya umeme na kushusha gharama za umeme. Kuna ubaya gani serikali ya Mama Samia, ikaondoa kodi zote kwenye ikiwemo VAT kwenye majiko ya gesi, umeme na gesi ya kupikia?. Mbona kwenye computes tumeondoa kodi?. Hawa Watanzania wenzetu elfu 22, wanaokufa kila mwaka kwa matatatizo yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, maisha yao yangeokolewa kwa matumizi ya gesi na umeme.

3. Wanasheria tuna msemo wa “exhaust local remedies” yaani kabla hujatafuta msaada wan je, anza na kile ulichonacho. Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiua nyoka, fimbo ya mkononi ndio uiwayo nyoka, kwenye huu mkakati wa rais Samia wa nishati safi ya kupikia, nishati ya gesi ni fimbo ya mbali, inayohitaji mitungi, na kusafirishwa, lakini kwa sasa zaidi ya asilimia 90% ya nchi yetu, tuna umeme, hivyo fimbo ya kweli ya karibu, ni majiko ya umeme, na sasa kuna majiko banifu ya umeme mdogo, ma rice cooker, na fryers, na pressure cookers. Serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya umeme wa kupikia, kama kwenye computers tumeweza, tunashindwa vipi kwenye majiko ya gesi na umeme?.

4. Serikali itambulishe ruzuku ya majiko ya gesi, umeme na mitungi ya gesi, kama ruzuku kwenye zana za kilimo na pembejeo ikiwemo mbolea. Enzi za Mwalimu, baadhi ya bidhaa muhimu zikiwemo, mbegu, mbole na pembejeo za kilimo, zilifanywa bei nafuu kuliko hata bei halisi kwa kupewa ruzuku ya serikali ili wananchi wamudu gharama. Kuna wakati wa uhaba wa maji, Tanesco ilikuwa inatumia gharama kubwa kuzalisha umeme wa gesi na mafuta na kuuza kwa bei ndogo kama ya umeme wa maji ili kutowabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama

5. Wafadhili mbalimbali wahamasishwe kujitolea kufadhili majiko na mitungi ya gesi kwa wasio na uwezo, wakiwemo TASAF iingize program ya kufadhili majiko, mitungi na ruzuku ya gesi kwa kaya masikini katika program yao ya kunusuru kaya masikini.

6. Tutunge sheria ndogo, by laws, kulazimisha taasisi zote za watu wengi, mashule, vyuo vya kati, vyuo vikuu, na mahoteli ni lazima kutumia ama biogas, ama gesi ili kuokoa mazingira na sheria za ujenzi zijumuishe njia za kesi kama ilivyo kwa mabomba ya maji, umeme na mawasiliano, watu walipe bili za gesi kama maji na umeme.

7. Ziwekwe tozo maalum kwa vibali vya mkaa, na ziwekwe faini kali kwa uharibifu wa misitu kutafuta kuni na uchomaji mkaa bila vibali. Kama Tanesco iliweza kuuza umeme kwa bei ya chini, na enzi za Mwalimu kulitolewa ruzuku kwenye bidhaa muhimu, na enzi za JPM, gharama za kuunganishwa umeme wa REA, zilikuwa ni Shilingi 27,000 tuu, na tumeshuhudia hadi vijumba vya nyasi, vimeunganishwa na umeme, hili linashindikana vipi kwenye gesi?.

8. Tuongeze matumizi ya mkaa wa mawe na mkaa mbadadala , na kuongeza matumizi ya majiko banifu.

9. Wenzetu walioendelea, gesi inasambazwa majumbani kwa mabomba kama maji na umeme, then vijiji vyote vinavyopitiwa na bomba la gesi, visambaziwe gesi majumbani kama ulaya, Tulielezwa itasambazwa hadi majumbani, kama Tanesco wameweza kusambaza umeme kote, maji pia yamesambazwa kote, TTCL inasambaza mkongo wa taifa hadi majumbani, kunashindikana nini kusambaza gesi hadi majumbani watu wakalipa bili za gesi kama ulaya?.

Mungu Mbariki Rais Samia aliweze hili la Nishati safi ya kupikia
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Ajabu huu uzi ungekuwa wa mapenzi au vijembe ungekuwa na post 1k huu uzi bora wa mwezi oct umechuniwa tu hili jambo kama ulitembea kwenye mawazo yangu naunga mkono hoja.
Safarini America...
 
Kwa macho yangu huu uzi ni yaleyale ambayo Serikali inataka kutupeleka kutumia Kodi zetu kama Ruzuku ili kuwapa faida madalali wachache wa nchini na wauza gesi LPG wa ugaibuni..., hii issue haiitaji Serikali kupigia chapio kabisa gesi (ambayo hatuzalishi) bali kuhakikisha nchi yenye kila aina ya chanzo cha umeme na asilimia zaidi ya 90 iliyounganishwa kwa umeme watu wanatumia umeme kupikia..., zaidi ya hapo ni kuchezeshwa mziki kama wanaserere....
 
Umeandika vizuri sana andiko lako.natamani watu wangelisoma lote kwa hakika wangebubujikwa na machozi ya furaha. Kama vipi andiko hili ungeweka kama makala pia ulisome kwenye vipindi vyako vya Tv na kutoa ufafanuzi huu .
 
Mkuu Pascal Mayalla sikutoa hio rebuttal hapo juu ili unipe like (hio like hata chukua).., nimetoa hio ili unielimishe ni vipi its a good idea kuchukua pesa ya mlalahoi ambae hawezi kununua kitu (gesi) eti ili tumpunguzie kwa kutumia pesa yake hio hio tulioichukua kwake..., ili tuongeze na pesa nyingine tuagize kitu kutoka ughaibuni ili tumletee huyu mlalahoi wakati kuna alternative hapahapa nchini ambayo ni way better....

Nadhani kuna kitu ambacho umekiona mimi sijakiona tafadhali nieleweshe.....; Point yangu ni kwamba kutumia hata kodi zetu kupunguza gharama ya gesi na majiko ya gesi bado ni utaahira logically..., (ingawa nadhani sio utaahira tu bali ni ubinafsi sababu kuna watu wanataka kutengeneza faida kwa mtaji wa mwananchi)
 
Back
Top Bottom