Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Private Public Partnership inafaa pale tu ambapo kuna mtu binafsi ana kitu ambacho serikali haiwezi kufanya, au anaweza kukifanya kwa ubora; Win Win Situation. Sasa katika Suala la Nishati Safi ya Kupikia kuna majiko ya kisasa ya Induction Cooker ambayo yana ufanisi wa percent 90; Yana Ufanisi zaidi ya mara mbili ya Jiko la gesi; Hivyo kwa mtu anayepikia tuseme kwa gesi kwa elfu sitini; ufanisi wa hili Jiko ni kama ataweza kupikia chini ya elfu 30 (Na hapo ni kwa gharama ya 192/= kwa Unit kwa mijini) kwa vijijini atakuwa ni kama anaweza kupika kwa elfu 10 (Gharama za Units kwa 100/=) kwahio, wakati jirani yake anatoa elfu 56 mpaka sitini yeye anatoa elfu 10/=
Gharama ya Majiko
Sababu teknolojia hii sio ya zamani sana hivyo gharama ipo juu kidogo kama watu watakwenda kununua madukani na pia inahitaji vyombo / chombo ambacho ni cha chuma (ferromagnetic) na sio sufuria za kawaida.
Nimeangalia kwa haraka haraka hapa nimeona majiko haya nchini ya plate moja yapo mpaka ya Tshs. 140,000/= (Ingawa kama tunaweza kutoa Mitungi bure huenda tunaweza pia kutoa ruzuku ya majiko haya)
Ushauri wa Partnership na Serikali / TANESCO
Kuliko watu kununua kutoka huko nje na baada ya gharama ya usafiri na faida yao hivyo bei kuwa kubwa; Tanesco inaweza kuingia Partnership na Kampuni ya kutengeneza majiko haya na kuagiza in bulk, au kuleta Assembly Plant nchini ili kuhakikisha kuna majiko ya kutosha na mtu wa kawaida anaweza kumudu Pesa za kuyanunulia.
Jinsi ya Mwananchi Atakavyolipa
Kutokana na kwamba TANESCO ndio atakuwa Msambaji wa haya Majiko anaweza akawapa watu kwa mkopo na kila anavyonunua Umeme wanakata Pesa yao ya Malipo ya Jiko hili kulingana na mtu alivyonunua.
Hii wanaweza kufanya sio kwa Induction Cooker pekee, hata vifaa vingine kama Multi Cooker, Rice Cooker, Jug Kettles, Blender n.k.
Hitimisho
Kwa kufanya hivyo wananchi watakuwa wameweza kuingia kwenye Nishati Safi, ya Kupikia kwa Gharama wanayoweza na Kama nchi Taifa tutakuwa tumejizatiti kwenye Usalama na huenda tukawa Taifa linaloongoza kwa Nishati Safi (Percent Kubwa from Renewable Energy)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza...