Nishati Safi ya Kupikia: Wiki ya Huduma kwa Wateja TotalEnergies Yamuunga Mkono Rais Samia, Kusambaza Gesi ya Majumbani Kila Kona Hadi Vijijini!

Pamoja na mazuri ya Total energies, wapokee simu yao ya huduma kwa wateja. Hata upige mchana kutwa hawapokei.

Pia, kadi za mafuta kila kituo Dar hakuna. Wanarushiana mpira tu, nenda kituo hiki...nao wanasema nenda kile.
 
UKWELI ni huo kwamba wapanga sera hawamo kwenye kuona unafuu wa bei ya umeme kushuka ndipo mahubiri ya nishati SAFI yawezekane. Vipato wanavyolipana ni VIKUBWA mno vimewapofusha hawavai viatu vya umaskini wa sisi wapiga kura wao !
 
Yaani lile andiko lilikuwa nzuri sana ni kiasi hawa viongozi wacopi na paste tu ila sasa ndio kwanza wapo bize na kampeni za makampuni ya gas ambayo gharama zake wengi wa wananchi hawazimudu kiuhalisia.
bei ziko detarmined na cotrolleled prices kama bei ya mafuta, umeme, maji na gesi, lakini bei
Ya mitungi na bei ya majiko
Is determined na supply and demand, serikali ikiamua
Seriously kutaka Watanzania tuachane
Na kuni na mkaa , inapaswa kuondoa kodi zote kwenye mnyororo wa thamani wa gesi, kuanzia majiko, mitungi hadi gesi yenyewe, na hata ikibidi kutoa ruzuku ya gesi kwa kaya masikini, wanapewa jiko bure, mtungi bure na gesi ya ruzuku ili gesi ndio iwe the cheapest option.
P
 
Namuona classmate wangu kwakwezi wote watoto wa forodhani pry school 😄
Ehe turudi kwenye mada,hizo mitungi wanasambazq dezo au

Ova
 
Anawadanganya tu hao Total energy mi nafahamu gesi zinazosambazwa uku bush ni za Rostam Aziz yaani Taifa Gas
Ni kweli kwasababu hawana mshindani, sasa baba la baba la vituo vya mafuta TotalEnergies kaingia gesi bwerere sio Taifa gas pekee!.
na tena zinawaendea wanachama WA CCM ambao sio wahusika na kuwaacha wanahostahili
Wahusika wanaostahili kutumia gesi ni wakina nani na hao wasiostahili ni kinanani na kwanini wengine wastahili wengine wastahili?.
nimeshuhudia mara kibao vikifanyika vikao vya CCM wilaya baada ya vikao wanagawiana mitungi ya gesi midogo ya Taifa Gesi tena ata mitungi mi 5 mi5 yaani Bora alivyotolewa Januari maana ngoja niishie hapo
Taifa gas ni kampuni binafsi iko huru kuwagawia gesi bure watu watu inaowataka. Hakuna ubaya wowote CCM kugawiwa mitungi ya gesi na wapenzi wa CCM, wapenzi wa Chadema pia wako huru kuwagawia gesi wanachama wao.
P
 
Namuona classmate wangu kwakwezi wote watoto wa forodhani pry school 😄
Ehe turudi kwenye mada,hizo mitungi wanasambazq dezo au

Ova
Duh...!, kumbe ni classmate wako!, kiukweli hii ni pisi kali halafu imesimama wima, always smiling hadi mtu unakosa pa kuanzia hivyo unabaki ... kwa macho tuu!, kumbe ni mtoto wa kishua wa Forodhani, secondari alienda wapi?.
P
 
Kweli kabisa mkuu.
 
Sijaona sehemu iliyoandikwa "Punguzo la bei ya gesi".

Kama unahamasisha watu watumie nishati safi huku bei yake ikiwa juu, hiyo ni Kazi bure.
 
Huwa najiuliza kama kweli viongozi wetu huwa wanajua namna ya kutatua matatizo.
Naona kampeni ya kugawa mitungi ya gas toka enzi za january akiwa waziri wa nishati, hii haliwezi kufanya watu watumie nishati mbadara na wala sio suluhisho.
Mtu unampa tungi wakati gas bado ni ghali, gas ikiisha atahifadhi mtungi arudi kwenye mkaa au kuni na mtungi anaweza kuuza kabisa.
Ni sawa mtu masikini umpatie gari yenye kubugia mafuta, na vipuri vyake ni vya ghali lazima baadaye atalipaki arudi kwenye usafiri wake au aliuze tu.
Solution wangekuja na namna ya gharama za gas kuwa chini kiasi kwamba mtu aone kabisa kutumia mkaa ni ghali zaidi kuliko gas. Hata sasa matumizi ya mkaa ni ghali lakini bado kubadilisha gas ni ghali kwa mtu ambaye anaacha kodi ya buku tatu kila siku.
Pia kuna jambo linanishangaza kwa watanzania, hata wale wenye kipato utakuta bado anatumia mkaa na gas kwa pamoja. Sijui ni maoea.
Mimi sina kipato kikubwa, nina familia ya watu sita na hata jiko la mkaa sina. Gas inapikiwa hadi maharage maana mimi naona mkaa ni expensive kuliko gas. Mtungu wa gas mimi hudumu siku 21-30 ule mkubwa kitu ambacho mkaa labda ningetumia wa 3000 kutwa ingezidi gharama za gas.
 
Hii kampeni ya nishati safi ya kupikia imekaa kibiashara zaidi na ninashaka ya itakakokwenda faida ya mauzo ya gesi, inaelekea kuna chama kinafaidika. Tangu kampeni hii ianze nimekuwa nikijiuliza kama kweli wanayo nia ya dhati watu waondokane na kuni na mkaa kwanini wenzetu wamejikita kwenye mitungi na majiko ya gesi tu? Hivi nishati safi ni gesi tu? Mbona hawasambazi majiko janja ya umeme? Mbona wanapenda kuwataka wafugaji na wanavijiji nao watumie mitungi ya gesi? Hili la wafugaji na wanavijiji kupewa mitungi ya gesi halikubaliki na ndilo linalokazia kuwa mpango wote uko kibiashara zaidi.
Mfugaji na mwanakijiji huko aliko anayo malighafi nyingi sana ya kujitosheleza kupata nishati yake ya gesi kutokana na mifugo aliyonayo bila kuingia gharama. Hapa kwa hawa wafugaji na wakulima sijaona wataalamu wowote wakijitokeza na kuwafundisha jinsi ya kutengeneza nishati hiyo, ambayo hawatakuwepo viongozi wa kupigiwa makofi kwa ukarimu wao wa kuwapa bure mitungi ya gesi.
 
Hapa umeongea ukweli sana mheshimiwa mayala nakuomba tu urudi tena jimbo la kawe safari hii tutakusomea dua nyingi ili upeleke wazo hili
 
Kama mawaziri na maprofesa ni machawq itakuwa wewe kajambanani
Kiukweli kabisa mimi huwa naumia sana kuitwa chawa!. Hivi chawa anaweza kupandisha bandiko lenye hoja kama HII ?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…