Tembelea sido kama walivyokushauri na ucheki utakachokiona kinafaa. Ni kitu ambacho mkeo akipende kukifanya sio kumlazimisha cha kufanya.
Kwa 1.5 million unaweza kuanzisha biashara kwa kuzingatia vifuatavyo:
1. Ni biashara gani inayotoka sana ambayo unaweza kuanzisha kwa mtaji mdogo
2. Fanya shughuli unayoipenda kwasababu ukiwa unafanya shughuli unayoipenda hata kama uko katika kipindi kigumu kibiashara unakuwa una motivation kuendelea kuifanya coz unaipenda.
3. Angalia matatizo yanayoizunguka jamii unapoishi na kutafuta solution yake. Hapo unapata idea ya biashara manaake mi naamini biashara ni kuisaisia jamii nayo inakulipa kwa solution unayoipa.
Biashara nazoweza kufikiria kwa haraka haraka ni hizi:
1. Kuanzisha duka dogo la kuuza vocha za simu. Hizi ni bidhaa zinazotoka fasta
2. Kwasasa kuna maeneo hawana umeme so wanategemea mishumaa. Anzisha biashara ya ketengeneza mishumaa nyumbani. Mtaji wake ni mdogo tofauti na watu wanavyofikiri. Jifunze kwa ku click hapa:
How To Make Candles - Step by Step - YouTube
How to Make a Candle: Step-by-Step Instructions for an Easy Candle - YouTubeHome made candles part 1 - YouTube
So nimekupa linki tatu wanatumia njia tofauti tofauti so chagua njia utakayoona inafaa au mix hizo techniques na kutengeneza ya kwako
3. Nunua pikipiki ufanye bodaboda (nadhani hilo ndo neno lake).
4. Anzisha biashara ya matofali ya kuchoma. Tafuta eneo mweke kijana awe anachoma matofali wewe unakuwa unaenda kutafuta wateja.
Nadhani hizo zitakusaidia.