Nishauri kuhusu hili wazo langu

proskaeur

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
1,571
Reaction score
4,924
Habari za muda huu wakuu

Mimi nataka nianze biashara Fulani ya kutembeza bidhaa mtaani kama machinga, ili kuvutia wateja nikawa nawaza niwe natembea na mzani wa kupimia uzito na mashine ya kupima blood pressure (nimesoma kozi ya Afya),, ninawaza kuwa napima bure bila malipo kwa kila mteja anaenichangia biashara yangu.

Ushauri na mawazo ninayoomba kwenu ni je hili wazo ni zuri na litaweza kunipatia wateja kwa biashara ninayowaza ya kutembeza mtaani, na pia hakuna usumbufu wa kupata kibali kwanza kabla ya kuanza kupima watu mtaani hasa suala la blood pressure, naomba wajuvi mnisaidie.

Nawasilisha
 
Mimi mgeni hapa lakini kuna funzo litapatikana ndani yake.
 

Kila jambo ni uthubutu, binafsi nakushauri ujaribu ili ujionee, ukisubiri kupewa mawazo huenda ukaja kukatishwa tamaa na walioshindwa maana WALIOSHINDWA WANA MANENO MENGI. Washauri wengine wapo mtaani watembelee ujionee nao wanafanyaje yao.
 
Kila jambo ni uthubutu, binafsi nakushauri ujaribu ili ujionee, ukisubiri kupewa mawazo huenda ukaja kukatishwa tamaa na walioshindwa maana WALIOSHINDWA WANA MANENO MENGI. Washauri wengine wapo mtaani watembelee ujionee nao wanafanyaje yao.
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri wako, but nimeamua kuomba ushauri maana humu pia kunaweza kuwa kuna watu walishawahi ama wanafanya hiki kitu na pia nilitaka kujua kama kuna uhitaji wa vibali hasa kwenye suala la kupima blood pressure maana humu kuna watu tofauti tofauti, nashukuru tena.
 
Wabongo wanvyoogopa kupima ata malaria ndo uwaambie blood pressure cjui kwakweli ila jitaidi Ujaribu.
Hahaha, ni kweli mkuu but sababu nina elimu hiyo nitajitahidi kuwa nawashauri kabla ya kuwapima mkuu maana BP haiusishi utoaji wa damu naamini wataelewa.
 
Kwanza nikupongeze kwa wazo lako ila vipimo kama kupima vital signs km pressure, temperature havihitaji kibali.

Kwa kukusaidia kuna taratibu za kutibu na kusaidia wagonjwa walio majumbani, umeruhusiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii unajulikana kama home based care. ( ucheki kwenye mtandao).
 
Ahsante sana mkuu, nitafuatilia.
 
Ni wazo zuri sana.

Kuhusu kupima BP hiyo haihitaji kibali. Pima pia uzito na urefu ili uwaambie na BMI. Thubutu Wala usiogope Cha msingi tu uwe na nyaraka za kuthibitisha kuwa unaweza kupima BP etc. Go ahead...
 
Ni wazo zuri sana.

Kuhusu kupima BP hiyo haihitaji kibali. Pima pia uzito na urefu ili uwaambie na BMI. Thubutu Wala usiogope Cha msingi tu uwe na nyaraka za kuthibitisha kuwa unaweza kupima BP etc. Go ahead...
Nashukuru Sana Kaka kwa kunitia moyo,, suala la BMI nililifikiria but kutokana na biashara nayopanga kufanya ni ya kutembea mtaani hivyo mzani wa kupimia urefu nitashindwa kuubeba maana ni mzito Sana, so sidhani kama kupima urefu nitaweza unless kama kuna namna nzuri ya kupima urefu bila kutumia weighing scale unaweza kunishirikisha
 
Wazo zuri kwa muda mrefu inafahamika kada ya afya ajira zipo na nimeshuhudia. Kwako vp? Au ni uamuzi wa kuwa mjasiriamali?

Wazo langu Bp pima bure ila uzito uwe unapima BMI hlf unatoa na ushauri wa lishe kulingana na hali ya mtu hlf unatoza buku. Hapa utajinadi kuwa unapima BMI na kutoa ushauri wa kitaalumu nadhani utapata wateja wengi
 
Asante Kaka,,, ajira ni Changamoto kote Tu hakuna afadhali kada yoyote Ile, nimefikiria ujasiriamali ili kuondokana na stress za kuwazia ajira

Pia kuhusuu suala la BMI nililifikiria Sana ila tatizo linakuja kwenye kupima urefu maana mzani wa kupimia urefu ni mzito Sana na Mimi biashara nayoifikiria ni ya kuhama hama kufuata wateja na sio ya kukaa eneo moja.

But kama kuna namna nzuri ya kupima urefu bila kutumia zile weighing scale za hospitalini ambazo ni nzito naomba unishirikishe ili niwe nafanya pia na kupima urefu, Ahsantee!!!
 
Una wazo jema sana,nakushauri anza na kitambulisho cha machinga kining'inize shingoni,piga kazi
 
Barabarani kuna watu wanapima urefu bila kutumia weighing scale, fanya kutembea ujione field mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…