Nishauri kuhusu saluni ya kike

Nishauri kuhusu saluni ya kike

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu natumaini mko wazima.

Leo niko mbele yenu kuomba ushauri kuhusu biashara ya saluni ya kike. Mimi ni kijana wa kiume mjasiriamali na popote penye fursa huwa siogopi kujirushiamo ila najua kidogo mno kuhusu hizi saluni za kike. Ila hapa jirani kuna mdada ambaye anasifika mno kwakipaji chake cha ususi na kaajiriwa saluni iliyoko mtaa wa jirani (Magomeni mapipa). Baada ya kufikiria nikaona kupitia kipaji cha huyo dada na mtaji wa wateja alionao niingie nae ubia kufungua saluni hiyo. Nawakaribisha kunishauri lolote kuhusu biashara hii kabla sijafanya chochote.
 
mkuu kama huyo dada anajulikana na watu, ongea nae muelewane then uingie ubia nae mkuu salon za kike zina lipa asikwambie mtu, me sister ndo kazi yake hiyo, na ukiangalia watoto wa kike siku hz full kusuka,kikubwa tafta sehem nzuri hata kama sehem ambayo hajulikan huyo dada then anza kazi maana akishasuka wadada wawili watatu wakipendeza lazma wenzake wakamsifie then atawaelekeza kwenye saloon yako waje nao kupendeza,! Wadau wengine watakuja,!
 
isak nashukuru sana kwa kunitia moyo
 
Saluni ya kike ni biashara nzuri na inalipa ila ukiwa wewe muhusika ndo unaujuzi na hyo biashara
 
Kama huyo dada anajua kazi ya saluni vizur fungua m nna vifaa vya saluni nauza
 
Fungua tu cha muhim ni usimamiz usimuachie sana huyo mdada hapo faida utaiona
 
Poa ndugu... nakubali kuwa biashara yoyote hupaswi kumwachia mtu/mfanyakazi 100% kwa kigezo cha kumwamini. Mashaka yangu ni kuwa hii biashara wateja wake ni wanawake na inahusisha mambo ya kike tu wakati mimi ni mwanaume.. ndo maana nimefungua uzi huu kupata ushauri wa kina kabla ya lolote.
 
Hakuna biashara ya kike wala ya kiume cha muhim ni nia ya kufanya hyo biashara na usimamiz wa kutosha,amin unaweza naamin utafanikiwa
 
Asante.. ntakucheki PM maana inaonekana unajua mengi kuhusu hili pia hivyo vifaa ulivyosema.
 
Kiukweli saloon yakike ni bonge la biashara,mm kipindi naanza kufungua saloon ya kike nilikuwa sina MTU hata wakunishika mkono lkn baada ya miezi kama miwili hiv nilijuta kutoanza mapema biashara hii ,chamsingi upate mtaalam wa kusuka vzr na site nzur nakuhakikishia ndani ya miez minne unafungua saloon nyingne tena.kikubwa usisite wala kukata tamaa
 
Mkuuu ulianza na mtaji wa bei gani Kwa kukadilia. .??
 
huyo mdada siku akiondoka na biashara unafunga?? hao wasusi wa saloon pasua kichwa sana
 
Back
Top Bottom