Mkuu Mtanganyika,
Kurudi kuishi nyumbani Tanzania kunategema na mambo mengi.
Je una mipango gani ya kibiashara kama unataka kufanya biashara ambapo inabidi(kwa tathmini yangu) uwe na paundi 100,000 kwa ku-set up biashara yako na kuanza kui-run. Hizo ni kwa maandalizi ya biashara yako ambayo pia inategemea ni biashara ya aina gani.
Lakini kama biashara ni kama duka, uuuzaji magari, kumiliki daladala, internet cafe, na mambo mengine kama hayo unahitaji pungufu ya hapo tuseme paundi 60,000.
Hapa kama unaishi Uingereza unaweza ukanunua magari makubwa yale ambayo ni used kwa less than £10,000 na ukaanza biashara na kuingia Kilosa na sehemu zingine.
Haya mambo yote ni provided kwamba tayari una assets kama nyumba umenunua au umejenga, gari ya kutembelea na fwedha benki ambayo inacheza kama paundi 20,000 na huigusi.
Pia unatakiwa uwe na hisa katika kampuni mbalimbali kama za simu,TBL, na kwingine.
Hivyo mkuu inabidi uwe na Business Plan ya nguvu ambayo ni siri yako na ndio biblia yako.
Unajua wenzetu wa West Afrika waloona mbali waliweza kufaidika na Ulaya ya enzi zile lakini kwa sasa inabidi uwe na maarifa zaidi, ya halali.