nishaurini jamani

korino

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
1,004
Reaction score
666
habari zenu wote humu ndani...mm ni mschna tangu nimeolewa ni mwaka mmoja tu! cjawah kugombana na mume wangu hata cku moja! nawapenda wifi zangu na shemeji zangu pia! jinsi ninavyoishi nao ni kama wadogo zangu kwan wananipenda na hawasiti kujakunitaka ushauri wa mambo mbalimbali! nampenda mama mkwe wangu km mama angu mzazi! tunaishi karibu karibu,,,mwendo wa km dk 10 kufika kwake! mara nyingi nnapenda kumpeleka zawadi ya vitu mbali2 km kuonyesha upendo na kudumisha udugu wetu! hata cku nnapopika chakula adimu huwa nampelekea anakula kwa furaha japo lazima atatia kasoro! lkn nimeshamzoea kwan ni mkorofi sana.

kitu km kunambia mimi mshenzi,cna adabu,najiona mzuri na maneno ya kebehi nimeshazoea kwake kwan maneno hayo hata matusi makubwa anawatukana hadi watoto wake! kwahyo huwa sion shida!

huyu mama alinipenda sana kabla cjaolewa na mwanae! alikuwa anasisitiza niolewe haraka sana kwan mwanae hatopata mwanamke km mm! hatimaye tulifunga ndoa.

maisha yetu kwa ujumla me na mume wangu ni ya kawaida sana! cri zetu tunazijua sisi wenyewe! tumelala njaa tunajua cc tukila vizuri tunajua cc!
chakushangaza mama mkwe ananisema sana kuwa mm jeuri sana, namwendesha sana mwanawe, na ni bora nicngeolewa na mwanae kwani cpendi watu, napenda maisha ya juu,ni bora mwanae atafte mke mwengine aoe! maneno haya nimeambiwa na wifi angu kabisa! na pia naweza kuamini haya kwani ckuiz akija kwangu anachunguza sana mpaka rum kwetu anaingia na makabati anafungua! juzjuz tu nilimfuma nafungua wallet yangu nakuipekuapekua!

yote haya cjamwambia mume wangu kwan naogopa mambo mawili 1.naweza nikawagombanisha mtu na mamake 2.naweza sema ntawagombanisha lkn kumbe kibao kikageuka kwangu nakuonekana mamake hana kosa sababu anampenda sana mamake!
jamani nyie acheni tu...huyu mama ana visa kwa kweli! ni vingi sana visa vyake!

sielewi nifanyenin naombeni ushauri wenu ndugu zangu
 
hapo ushauri ni kuhama
kwenda kuishi mbali na huyo 'mwehu'

hivyo sio visa
huyo ni mgonjwa.....mumeo angekuwa muelewa
mngempeleka hospitali kwanza
 
Vumilia tu, mvumilivu hula mbivu.
 
Endelea na uvumilivu wako, huku ukimshauri mumeo kuhama kama mmepanga.

Pia anza mtindo wa kufunga chumba chako, mmeo awe na copy ya funguo.
 
hapo ushauri ni kuhama
kwenda kuishi mbali na huyo 'mwehu'


hivyo sio visa
huyo ni mgonjwa.....mumeo angekuwa muelewa
mngempeleka hospitali kwanza
fata ushauri wa the boss hakuna kingine
 
tatizo hukuweka mipaka toka mapema, ulipaswa kumheshimu na kumpenda mama mkwe na si kujifanya mtumwa.

Ukianza kuiweka mipaka sasa lazima utaonekana mbaya, lakini haina tatizo wanasema 'mbwa ukimjua jina hakusumbui'
madhali unajua tabia ya mama mkwe wako mchukulie jinsi alivyo.....

Kuhusu chumbani kwako.......
Ni vyema ukawa unafunga na funguo funguo tembea nayo kiunoni..... Na unapomuona anatenda ndivyo sivyo muambie hapo hapo...

Kiafrica haifai mzazi kuingia chumbani kwa mwanao aliyeoa au kuolewa....
Sasa badala ya kulalamika jf, akifanya hivyo mueleze wazi kuwa hupendi..... Na usimtuhusu kuingia chumbani

akipekua pochi yako muulize alisahau nini kwenye pochi yako.....
Yes, atakusema na kukuchamba lakini ujumbe utamfikia.

Take control of your house, usimtukane wala kumdharau ila mweleze ukweli anapovuka mipaka
 
shukran kaka..hicho kitu pia nlikiwaza! lkn namwomba Mungu kwanza nipate kazi mkoa wowote ule ili hata tukihama tunajua mshahara upo! siwez ondoka kwa sasa maana itabidi mume wangu aache kazi so maisha yatakuwa magumu! alikuja kwangu cku moja akamkuta babake mzazi(ananipenda sana huyu mzee) nimemtayarishia chai nzuri tu! basi alinifokea kwann nimemwekea juice nyingi na keki! ndomana watu wanapendakuja sana nyumbani kwangu so ctokuwa na maendeleo! nlimckilizia nkamwitikia sawa mama nimekuelewa! ana visa sana
 
huwa nafunga dada nkiwa nimetoka lkn km hivi nipo tu nausindika tu sababu nakuwa naingia mara natoka!thx
 

mradi unajua tabia mchukulie jinsi alivyo kikubwa usimpe access ya chumbani kwenu na asijue mambo yenu.............. Akikukwaza mwambie.............
 
unajua nini kisa cha mamamkwe kumchukia mkwe wake ni kwamba anona unafaidi vya mwanae,kumbuka kabla mumeo hajakuoa alikua anatoa msaada mf:hela kwa kiasi kikubwa sasa baada ya kua na familia msaada umepungua na ni kwa sababu gani ni wewe ambaye unaonekana unahinder lakini we kua mvumilivu mheshimu na mpotezee hayo maneno yake yaani ucjali hata akiongea hata ukisema utahama maneno bado yatakuwepo yamenitokea lakini nashukuru Mungu mume wangu anawafahamu ndugu zake na wewe unatakiwa utafute jinsi ya kumweleza coz mume wako akija kusikia we ndo utaonekana mwenye makosa unakumbuka ile thread ya ka Kakiiza alikua anamlamlamikia mke wake angalia yacje yakakupata ni hayo tu
 
mnh kuolewa si kazi,kazi kulea ndoa....
huyo mama ana ukichaa unaoambatana na old age nadhani,fuata ushauri wa Badili Tabia....ukiona haelekei mzibue vibao lol lolote na liwe....tell her you have enough problems and you dont need extra lol
 
thx ndugu yangu! cku ile alipofungua walet yangu nlishtuka na kujikuta namwambia "hapana mama usifungue ifunge" akacheka anasema unaogopa nn???unadhan ntakufumania! da! nlikaa kimya tu
 
huwa nafunga dada nkiwa nimetoka lkn km hivi nipo tu nausindika tu sababu nakuwa naingia mara natoka!thx

sasa ukimsikia anagonga tu kimbilia funguo funga chumbani kwako then mkaribishe kwa bashasha
 
thx ndugu yangu! cku ile alipofungua walet yangu nlishtuka na kujikuta namwambia "hapana mama usifungue ifunge" akacheka anasema unaogopa nn???unadhan ntakufumania! da! nlikaa kimya tu

usikute mshirikina huyo mama...
ukimuendekeza utajuta....kuwa tough...
 
sasa ukimsikia anagonga tu kimbilia funguo funga chumbani kwako then mkaribishe kwa bashasha

hana haya huyu! anasema kabisa nataka niingie chumbani kwako! anasema saingine nataka niende toilet lkn ctak toilet ya nje nataka ya chumban kwako!
 
usikute mshirikina huyo mama...
ukimuendekeza utajuta....kuwa tough...

kwa ushirikina ndo mwenyewe haswaa! anayapenda sana! amemloga mumewe hadi basi lkn Mungu mkubwa atanisaidia
 
hapo ushauri ni kuhama
kwenda kuishi mbali na huyo 'mwehu'

hivyo sio visa
huyo ni mgonjwa.....mumeo angekuwa muelewa
mngempeleka hospitali kwanza

lkn anaonyesha kunipenda sana na kuninyenyekea tukiwa na mume wangu au watu wengine! huwa ananishangaza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…