Nishaurini kuhusu biashara ya viatu wakuu

Nishaurini kuhusu biashara ya viatu wakuu

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Wazima ndugu zangu?nataka nianze biashara ya viatu vya mtumba ila classic

Sitaki nianze na vingi nooh nataka nianze na pcs 3000 kwanza

Location nitatafuta eneo lenye hekaheka na shughuli nyingi

Nishaurini ninini cha kuzingatia?
Hii biashara imekaaje?
Jee inalipa?
Ununuzi jee
Changamoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazima ndugu zangu?nataka nianze biashara ya viatu vya mtumba ila classic

Sitaki nianze na vingi nooh nataka nianze na pcs 30 kwanza

Location nitatafuta eneo lenye hekaheka na shughuli nyingi

Nishaurini ninini cha kuzingatia?
Hii biashara imekaaje?
Jee inalipa?
Ununuzi jee
Changamoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
Viatu vya kiume vya mtumba ni biashara yenye faida kubwa Sana

Mambo ya kuzingatia siyo mengi Sana
Ni machache tu kama upo mwanza
Kama mimi unaenda pale lango moja
Ndio sehemu vinapatina viatu vya mtumba
Vizuri na kwa bei nzuri

1 kuwa makini kukikagua kiatu unachochukuwa vizuri kwasababu kuna viatu vinakuwa vimearibika hivyo usipo chagua kwa makini utauziwa hivyo hivyo kwa bei juu itakupa hasara ya kwenda kukirekebisha

2 zingatia namba kubwa nyingi na zakati ili nalo ni muhimu kwasababu watu wengi waofika bei nzuri bila usumbufu ni wenye miguu mikubwa kwasababu viatu vyao ni kazi Sana kupata size zao kwaiyo ukiwa na size kubwa kiatu umekinunu 10 siyo ajabu kuuza 30

3 Jitaidi kuchagua viatu ambavyo ata wewe mwenyewe unavipenda ni muhimu sana kuchagua viatu vizuri kwasababu kizuri akitakupa shida Sana kumshawishi mteja mtu kitamvutia tu atakuita yeye mwenyewe

4 Jitaidi kuwa mchangamfu kwa wateja na kumuonyesha viatu mbalimbali hii inaweza kumshawishi mteja akuchangie ata kiatu zaidi ya kimoja

5 Ili ni la mwisho japo yapo mengi sana Jitaidi kuwa na nidhamu na msafi na jiepushe kuwapa wateja majibu mabaya kwasababu wateja wako na tabia mbalimbali wako watakao kukera wewe jitaidi kumjibu vizuri tu ili utimize lengo lako la kupata pesa yake
Nakutakia kazi njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom