Nishaurini kuhusu Nissan Pathfinder

Kuna ambazo zinauzika lakini generation ya pathfinder Terrano na X-trail kuna shida
Terrano si ndio hio hio pathfinder kwa marekani mkuu, anyway navyojua ni gari nzuri yenye nguvu ila inaleta presha sana kama mtumiaji ukiwa huna vyanzo vizuri vya mapato.

Early 2007 tulikuwa na terrano wakati ziko kwenye peak apa kibongo bongo ila spear zake ndio ilikuwa mtihani mkubwa hasa suspension zake zilitutesa mno. Hii gari parts nyingi ni electronic controlled so ilikuwa na issues za kukausha battery at times ikikaa idle. Mashine yetu ilikuwa ni V6 r3m it was thirsty ile mbaya hivyo nategemea pia hilo toleo la pathfinder litakuwa na Engine ya V6 ikiwa na zaidi ya 3000cc, hivyo mtoa mada ajiandae na gharama za kutia wese mara kwa mara.
Uzuri ni kwamba gari hio gari inabembeleza mno ukiwa ndani, starehe yake haielezeki aisee...Ni nzuri sana kuiendesha na ina nafasi ya kutosha ndani.

Hivyo kwa mtoa mada jitathmini pumzi yako kwa hio pathfinder ikiwa ni maandalizi mazuri ya running and maintainance costs. Otherwise unaweza ukafanya tu choice nyengine mkuu klins
 
Nissan terrano ni gari nzuri sana lakini ikiharibika dah kichwa kinauma!

Tangu ninunue hii gari sijawahi jutia kuhusu mafuta but kichwa kinawaka moto pale ikiharibika😅😅😅😅 kugusa tu spare tu laki 5 kawaida.

Na kuzipata taabu sana nakumbuka kuna kipindi nilizunguka kariakoo mpaka nilichoka kupata spare zake...
ila ni gari ya shuruba sana kwakweli.
 
Gari nzuri sana,engine ndogo kwa gari ya caliber yake 2.5i diesel na ina turbo,mbio ndio zimelala kama unapenda mbio unachanganya faster,na nisix speed,shida yake ni spare,ikizingua unapark,ziagizwe japan/Thailand,ila sio gari ya kuharibika hovyo pia,maana ni level ya ford everest,toyota fortuner.
 
daah umenitamanisha sana mkuu new model sijui zitakuwajee!? maisha haya



PATH FINDER
 
Haina tofauti na NISSAN NAVARA kwenye spares(zinaingiliana)....spares zipo ila bei ni juu kidogo ukilinganisha gari ambazo wengi wamezoea kama rav4,corolla
Kaka vipi land rover 2012 hizi new model ,una ushauri gani hapo? Nataka kuagiza.
 
Gari naipenda sana hii, very very comfortable
 
Embu sema uliiuza sh ngapi?
resale value yake ikoje maana juzi nimekuona unaendesha bodaboda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…