Nishaurini kwa hili

mkazamjomba

Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
61
Reaction score
21
jirani yangu ana tabia ngumu sana mie huwa nina tabia moja kwa vile ni mfanyakazi ninapokuwa siendi kazini sina muda wakwenda nyumba za watu ila kama msiba au ugonjwa nashiriki vizura maana mara nyingi nakuwa bize sana na majukumu kama mama sasa anachonikera anangoja nikiondoka tu ana kazi ya kuomba vitu msichana wangu wa kazijuzi asubuhi nilichelewa kuondoka nilipitia hospital hakujua kaja kuomba sukari nikatoka ndani alijipurukusha nikamwambia kwa nini shida zako huniambii mimi ninayetafuta oh samahani niliishiwa sukari nikamwambia hujaanza leo sasa kama una shida sitaki umwambie huyu binti ameninua ana sema nina ringa anamsema hivi huyo mamako akiacha kazi si atakoma nashangaa maneno yametoka wapi na majirani wote hawana nae uhusiano mzuri ila nahisi msichana wangu ana kahusiano ka siri ametengeneza urafiki fulani ni nifanyeje? nishaurini kwa busara zenuKWA
 
kwanza kabisa maisha nikusaidiana,pili leo utakuwa nacho kesho hauna na ww cku ukiwa hauna nani atakusaidia ?,tatu usiangalie watu wanamchukuliaje huyo mama, ila mweleze tuu kiustaarabu kuwa ukitaka kitu niambie mimi kwanza ili ww ndo umruhusu huyo housegirl,alafu usipende ugomvi na majirani!
 
kwani sababu ni hiyo ni kwa nini haniambii mimi msichana aliyeondoka walijenga urafiki na aliiba sahani akaficha kwake matokeo hakumpa wakakosana ninaogopa mazoea ya kuhamisha vitu ndani
 

good woman,...............Mungu akubariki
 
kwani sababu ni hiyo ni kwa nini haniambii mimi msichana aliyeondoka walijenga urafiki na aliiba sahani akaficha kwake matokeo hakumpa wakakosana ninaogopa mazoea ya kuhamisha vitu ndani

unaonekana ni mkorofi na mbinafsi saaaaaana,...ushauri ni kwamba_badili tabia na huo mtazamo wako juu ya wengine,..utafurahia maisha
 
unanielewa vibaya ndugu yangu tatizo kila mtu yuko kwake sio nyumba ya kupanga lakini nadhani hujawahi kukaa na jirani dizaini hii anayejenga mahusiano na housegirl? haji kwako ukitoka tu kaja mimi nataka hata nikiwepo eje kama ni shida umsaidie walishirikiana na housegirl kuficha sahani zangu inamaana wasingegombana nisingejua
 
dada! msamehe unajua binadamu tunatofautiana katika kuwaza, hivyo msamehe kwa moyo mmoja alafu umwite ndo umweleze kuwa haupendi hiyo tabia lakini ukiweka rohoni utazidi kutenda dhambi na utajizibia baraka zingine kwa Mungu!
 
Kwa nn asikufuate wewe mwenyewe huyo mama nae ana matatizo inaonekana hiyo ndo tabia yake ya kuomba kuomba.Sasa anaona aibu akikufuata wewe ndo maana ameleta mazoea na msichana.Cha kufanya mpige mkwara huyo msichana kama hujaona ako katabia kana isha.Na wala mtu asikutishe pesa utafute mwenyewe halafu umlee mtu kipuzi puzi
 
Kaa na msichana wako muonye kwa upole pia asiwe kalibu na huyo jirani na asipokuelewa bas achana naye tafuta mwingine
 
Mmmh kama wewe unania ya kutoa toa tu bila ya yeye kuja kuomba wewe. Usisahau ile methali inayosema, Akupigae kofi shavu la kulia mgeuzie na kushoto. Kama unahisi kuna uhusiano si mzuri wa kumwonya ni housegirl.

Toa mama utabarikiwa, dada huyo njaa hana lolote.
 
Wewe ni mshari,kama ulijua ana hilo tatizo ungemweleza sio kumvizia kila mtu ana mapungufu yake.Ongea nae tena kama mama mwenye akili
 
Aisee nilikuwa na binti design hiyo, sukari, mafuta hadi mboga. Inaudhi? Weekend huoni mtu wa kuja kuomba ila weekdays; budget yaharibika sana!
 
Usimwambie jirani yako nenda halafu urudi hali unacho anachokihitaji,
'mithali....,
huyo beki tatu wako sio kiungo kizuri kati yako na majirani,
huenda anaeleza pia mambo ya ndani kwa hao watu,kama mazingira yenu yanaruhusu kushare vitu namna hiyo go on, kama sio basi hao ni wezi tu,
so liangalie vzr hilo
 
Pole, ninavyoona hiyo tabia yako si nzuri kutowajulia hali majirani hao ndio ndugu zako wa karibu usingoje misiba na ugonjwa, jirani wamejenga ukaribu na msichana kwasababu wewe unajifungia na kuwa bize. Na umejuaje kwamba huyu jirani hana mahusiano mazuri na wengine? au hisia zako tu? Na kama una mahusiano mazuri na msichana wa kazi angekwambia kila kitu. Ushauri wangu weka mahusiano mazuri na jirani, badirika, yakikukuta ya ugonjwa na msiba utajua gharama yake..
 
women affairs.....sijui kwanini mnazoeana kihivi

kwa mimi nazani huko sawa kukataa mazoea na majira wasio na mahusiano mazuri na majira wenzao cha kukushauri mkataze msichana wako na huyo bibi kwa kutakuja kuleta matatizo ktk nyumba yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…