nishaurini nipande zao gani

nishaurini nipande zao gani

yaser

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
1,361
Reaction score
299
wanajamii habarini za muda huu na poleni sana kwa majukumu ya kimaisha......napenda kuwauliza ni zao gani ambalo linaweza kustahimili kwenye ardhi ya mchanga hasa kwa kipindi hiki ambacho kwa hapa dar-es-salam kuna mvua za hapa na pale.
nitashukuru kwa majibu yenu pia nawatakia kazi njema na mungu awape afya tele na maisha mrefu mzidi kusaidia jamii yetu
Ahsanteni sana
YASER.
 
unataka kulima hapa dar?....maeneo gani labda.......otherwise sidhani kama hapa dsm ni sehem sahihi ya kulima zao la maana
 
mihogo ila tafuta mbegu nzuri, sina uhakika unataka uvune lini, ngoja waje wataalamu hapa
Malila, Kubota, Mama Timmy
 
unataka kulima hapa dar?....maeneo gani labda.......otherwise sidhani kama hapa dsm ni sehem sahihi ya kulima zao la maana
ni dar maeneo ya kigambon njia ya kuelekea kimbiji
 
Tazama mashamba ya jirani wanalima kitu gani kinachokubali maeneo hayo. Kilimo kinategemea ardhi na hali ya hewa ya maeneo husika. Kama ufuta unakubali maeneo hayo, nakushauri ulime zao hilo ktk msimu wake kwani bei yake ni nzuri sana siku hizi.
 
Panda mazao ya kudumu kama michungwa, minazi, miembe nk. Kwa kifupi panda matunda. kama unataka kupanda mahindi basi panda ya miezi mitatu au miwili. Lakini miti ya matunda ndio the best kwa Dar.
wanajamii habarini za muda huu na poleni sana kwa majukumu ya kimaisha......napenda kuwauliza ni zao gani ambalo linaweza kustahimili kwenye ardhi ya mchanga hasa kwa kipindi hiki ambacho kwa hapa dar-es-salam kuna mvua za hapa na pale.
nitashukuru kwa majibu yenu pia nawatakia kazi njema na mungu awape afya tele na maisha mrefu mzidi kusaidia jamii yetu
Ahsanteni sana
YASER.
 
Mkuu maeneo hayo ni maarufu kwa viazi vitamu, kama unayo maji na mbolea panda nyanya, pilipili aina zote, bamia na spinachi.
 
unataka kulima hapa dar?....maeneo gani labda.......otherwise sidhani kama hapa dsm ni sehem sahihi ya kulima zao la maana

Du kweli wewe utakuwa mtu wa ofisini sana,yaani Dar hakuna sehemu ya kulima zao la maana kweli.Temeke kuanzia Mbagala Rangi Tatu mpaka Vikindu unaweza ukalima mihogo, mahindi, maembe na pia mananasi. Na sehemu zingine za Dar unaweza ukafanya kilimo chochote cha umwagiliaji na ukajipatia riziki
 
ni eneo la ukubwa gani na kwanza umejiandaaje nikimaanisha kihuduma na pia kimasoko unao muda wa kusimamia hayo yote?
 
Back
Top Bottom