Umefanya vyema kuzingatia msimamo wako na kuondoka, ungeonyesha unyonge mkubwa sana kama ungebaki hata baada ya kutishia kuondoka. Ujue kila alichofanya alikuwa anakujaribu tangu simu ya mwanzo, tatizo hukugundua na hukuonyesha msimamo imara hata baada ya kuona hutoliwahi gari. Ile ya kwenda kumsaaidia kufua ungeipotezea, yy alikuwa anatakaa wende tu ukamuone na akusimulie mambo ya Club yalivyokuwa na kukupima kama uta-ract vipi. Sasa mie nakushauri, uwe na misimamo katika maamuzi yako, na hiyo itakujengea heshima, mfano punguza kupiga simu kwake, na usizime simu yako ukiwa huru iache tu akipiga msikilize. Na usikubali akuvute upande wa tabia yake: Acha utani ambao hauna maana, mjengee msimamo.