Hovering
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 275
- 912
Waungwana habari za muda, naamini tu salama na wazima wa afya, kama unachangamoto pole na Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi na itapita.
Nimeandaa uzi huu kama sehemu ya kusaidia vijana wa kiume na hata wakike pia ili waweze kuepukana na hatima za huzuni, mathalani KATIBU ANAYETREND KWA WAKATI HUU (KIFO CHA KATIBU).
Yapo mambo machache sana ambayo unapaswa kuyafahamu ili kuepukana na visa kama hivi vya kujitoa uhai kisa mapenzi. Hapa tuelewane, vijana wakiume wanaathirika zaidi na mahusiano ya mtindo huu (mke wa mtu/jimama), na hii ni kwasababu kuu tatu ambazo zinaweza kuelezeka katika mazingira tofauti tofauti.
CHANZO CHA MAHUSIANO (LOVE SOURCE)
Mahusano ya kimapenzi baina ya kijana na mama mtu mzima au mke wa mtu huanzia au kuchochewa na wanawake wenyewe kabla ya kijana kujikuta katika dimbwi zito la hisia. Japo wapo vijana baadhi ambao huwaanza watu wazima.
Katika uhalisia na ukweli wa mambo ni kwamba, wakati huu wote huwa hakuna upendo wa dhati kutoka kwa chanzo cha mahusiano (mke wa mtu), zaidi ya tamaa za kimwili au lengo la ziada.
Kijana kutembea na mke wa mtu au jimama mara nyingi haitokei kwa bahatiyaani (coincidentally), bali kusudi (intentionally). Sifa kadhaa za kijana huwa ni chachu kwa mwanamke huyu kuvutika na moja wapo ni UTULIVU NA UKIMYA.
Naelewa unafikiria suala la unadhifu au smartness lingeanza lakini kiuhalisia mtu mtulivu na mkimya hawezi kuwa ROUGH kama neno linavotumika mtaani. Hapa yapo mengi ya kuongelea, naamini tutayachambua vizuri katika nyuzi zijazo lakini la utilivu na ukimya ni credit kubwa.
MAAMUZI NDANI YA MAHUSIANO
Tunapogusia maamuzi, hapa kinachomaanishwa ni namna kijana anaweza kupata access ya chochote kutoka kwa huyo mke wa mtu au jimama kuanzia mwili wake (sex) mpaka mali zake (gari, nyumba na pesa).
Wapo baadhi ya wake za watu ambao wanaenda mbali zaidi na kutaka kuifahamu familia yako na hata kukupiga jerk inapotokea kuna tatizo la kifamilia linalohusiana na pesa. Kwakuwa vijana wengi bado ni watafutaji, wanapopewa pesa na offer mbalimbali na wanawake wa type hii huwa wanazama zaidi na kuongeza upendo wakiamini offer hizi ni matokeo ya upendo wa kweli kutoka kwa wanawake kitu ambacho sio sahihi.
Kwasababu mwanamke huyu anakuleta katika 18 zake, sasa inabidi akupe nafasi kubwa na kukuonesha dhahiri kwamba unapendwa na umri au status yake ya ndoa siyo kigezo cha nani anastahili kuwa mfanya maamuzi ndani ya mahusiano. Hapa sasa ndiyo hapo tunaipata point ya mpendwa wetu Katibu, UPENDO WA KWANZA AU MWANZO ULIYOPOTEA NA KUFANYA AJIUE.
UGUMU WA KUJINASUA KUTOKA KWENYE MTEGO
Hii ndiyo chanzo cha matukio yanayoweza kupelekea maamuzi kama ya mpendwa wetu the late Katibu. Pasi na kujua kwamba lengo la wanawake wa type hii ni kutimizia haja zao wanazozikosa kwa watu wao halali(mume).
Basi kijana anajikuta amekuwa tegemezi kuanzia hisia, maamuzi na mali pia. Kijana anapoanza kuona ishara za kupotea attention (UPENDO WA AWALI/MWANZO ) ya mwanamke hapa ndio tatizo huanzia.
Katika hali ya kawaida mahusiano haya mara zote huwa ni siri baina ya wahusika, changamoto hii inapotokea kijana hulazimika kuumiza kichwa na moyo wake mwenyewe bila kumshirikisha mtu kwa maslahi ya privacy yao wote.
Kwahio wazo lolote litakaloonekana kuwa suluhu kwa wakati huo basi atalipa nafasi. Ikumbukwe aina hii ya mahusiano mwanamke (mke wa mtu/jimama) huingia akiwa anajua hatima au mwisho wa mahusiano ni baada tu ya kutekeleza agenda yake nahii, hufanya asione shida kuchana mkeka maana hataumia ukilinganisha na kijana aliyepo mtegoni.
Kwa wewe kijana, mke wa mtu au jimama ni kweli yapo mazuri ya kupumbaza unayoweza faidika kutokana mahusiano ya aina hii, lakini mwisho wa yote mzani huegemea upande wa hasara.
Karibu PM kwa ushauri.