Nisome chuo au Advance

Nisome chuo au Advance

Mi wacha nikushauri kwa faida yako na wengine.
Kama wadau walivyosema hapo juu (mi sina uhakika) ni kwamba ukisoma EGM huwezi enda Engineering. hilo la kwanza tilia maanani.
Mi ninachokiona hapa ni kwamba unaweza tu kuhamua either kwenda 'advance' au kwenda chuo, yote ni sawa tu. Ila ujue kwamba kuna faida na hasara za kila option. Ukiamua kwenda 'advance', maana yake uwe tayari kufanya national form six exam na kufaulu ili uweze kwenda chuo. Faida ya option hii ni kwamba unaweza maliza form six na ukagundua kwamba hautaki tena kuwa engineer, hivyo ukabadili fani na kusoma kitu kingine chochote upendacho. Mfano EGM unaweza kusoma degree ya Accounts, Business Admin, Finance, IT, Economics etc. Hasara yake ni kwamba ukimaliza form six, na ukafeli, unakua huna profession, yani huwi mtaalamu wa kitu chochote. Tofauti na ukimaliza diploma ambapo unaweza kutumia cheti cha diploma kuombea kazi sehemu husika. Hasara ya kwenda diploma ni kwamba utatumia miaka mitatu kupata diploma, wakati advance ni miaka 2. Pia, ukishakua na diploma ni vigumu kidogo kutumia cheti cha diploma hiyo kuomba kozi nyingine chuo. Mfano, kama una diploma ya I.T, huwezi kuitumia kuomba degree ya Accounts!
 
Mdogo wangu mimi ninakushauri ukasome Chuo kusoma 5&6 wakati mwingine ni kupoteza wakati kwa mtu anaefahamu nini anacho kitaka katika maisha. Itakuwa rahisi kwako kwenda chuo kikuu ukiwa tayari kwa ajira au umeajiriwa lakini pia nakushauri uangalie chuo kama DMI kina ajira za moja kwa moja kama ukisoma hapo.

DMI ndiyo kipi hicho?
 
ukienda chuo kusoma engeneering itakuchukua miaka mi3 kupata diploma ya civil alaf baada ya hapo ndio uchukue degree ambayo ni miaka mi4 kwahyo hapo jumla utakua umetumia miaka 7...
Ukienda advance miaka mi2 then degree miaka mi4 jumla miaka 6 so utakua umesave mwaka
acha kudanganya watu wewe!!!! KAMA HUJUI SI UULIZE???? ukiwa na diploma huwezi soma engineering miaka 4 hata siku moja!!!! hapo ni miaka mitatu tu!!!! upo??? ila kama ukitokea fom6 ndio unasoma miaka 4 na mara nyingi mwaka wa kwanza huwaga ni basic au introduction ya engineering na mara nyingi masomo yanafanana kwa kozi zote!!!! diploma ya engineering kwa nnavyojua ni miaka 2 sasa sijui unamaanisha nini??!!!
 
nakushauri uende chuo coz me mwnyewe yalinikuta km wewe, nilimaliza form 4 2007 nkapata 1 point 14, nkachaguliwa chuo bt wazazi wakaamua kunipeleka advance. 2010 nmetoka na 3 tena ya mwisho yani point 17 so me ushaur wangu nenda chuo kama umepangiwa huko.
 
its pocbo unaweza kusoma EGM na ukachukua civil engineering.Nakushaur nenda advance level kwanza
 
nakushauri uende chuo coz me mwnyewe yalinikuta km wewe, nilimaliza form 4 2007 nkapata 1 point 14, nkachaguliwa chuo bt wazazi wakaamua kunipeleka advance. 2010 nmetoka na 3 tena ya mwisho yani point 17 so me ushaur wangu nenda chuo kama umepangiwa huko.

Bado post hazijatoka ila na uhakika nitapangiwa chuo coz ndipo nilipochagua kama 1st selection
 
Back
Top Bottom