Nisome masomo gani ili nije kuwa Mhandisi?

Nisome masomo gani ili nije kuwa Mhandisi?

Matata25

Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
60
Reaction score
18
Wadau mimi ni kijana nilikimbia shule nikiwa form one but now naitaj kurudi school november 13th ila nitasoma QT na ndoto yangu ni kuwa Engineer wa electronics zote i mean computer na vifaa vinginevyo vinavyoendana na technology TV's phones consoles etc...

Wasomi ni wengi humu Jamiiforums please naomba ushauri nifuatilie masomo gani, ili nipate njia rahisi ya kutimiza ndoto yangu.

Natanguliza shukrani na mchango wenu ni muhimu kwangu
 
Hesabu sana na physics kwa ajili ya kubalance ingawa physics baadae hutokuja kuitumia. Jitahidi kujua hesabu mkuu. Hongera kwa wazo la kurudi shule.
 
Kama walivyotanguliza wadau hapo juu mambo ya hesabu ili kuchangamsha fikra ila nitaongezea pia umuhimu wa kuwa karibu na unachotaka..jiweke sana karibu na vitu pamoja na watu ambao wako unapotaka kuwa ndio utapata maarifa zaidi maana mwisho wa siku daftari huzidiwa na maarifa katika utekelezaji. Ni maoni yangu tu.
 
Physics chemistry basiic maths ukishafaulu qt yako..mwakani soma masomo haya kwenye private candidate yako..physics,maths,chemistry english language na civics halafu ukifaulu nenda diploma ya ufundi dit,mbeya ,arusha au st.joseph..baadae utasoma degree ya engineering sawa..
Pambana..
 
At the end God will ask you ''How Much Efforts Have you put onto what you Did & Like ? ''

Pambana kijana na hayo masomo waliyozungumzia wadau hapo juu !
QT ni tough kidogo put much efforts !
 
Wadau mimi ni kijana nilikimbia shule nikiwa form one but now naitaj kurudi school november 13th ila nitasoma QT na ndoto yangu ni kuwa Engineer wa electronics zote i mean computer na vifaa vinginevyo vinavyoendana na technology TV's phones consoles etc...

Wasomi ni wengi humu Jamiiforums please naomba ushauli nifuatilie masomo gani, ili nipate njia rahisi ya kutimiza ndoto yangu.

Natanguliza shukrani na mchango wenu ni muhimu kwangu

Kijana kwa kuwa mwanzo wa safari yako ni kuanzia kidato cha kwanza ni vyema ukazingatia masomo yote kwa usawa...

Kwa namna mfumo wa elimu ya sekondari Tanzania ulivyo, ufaulu wa jumla ni muhimu kuliko ule wa somo moja moja...

Lakini wakati ukiendelea kusoma hakikisha unaweka mkazo kwenye masomo ya hisabati, kemia, fizikia na kiingereza (somo hili ni muhimu kwa kuwa lugha mama ya ufundishaji ni umombo)...

Elimu ya A-Level ni muhimu kwako na mchepuo wa PCM ndio sahihi kuelekea ndoto yako.

Kwa elimu ya chuo kikuu ni vyema kama utaviepuka vyuo kama UDSM, UDOM kwa kuwa havimuandai mwanafunzi kufanya elimu kwa vitendo.

Honestly DIT ni sehemu nzuri kuliko hata UDMS, UDOm & co.....
 
Ushauri wa uongo huu....

Huwezi kuitenga engineering na physics hata siku moja...

Asante mkuu mkuu yaan nimefikiria huyu jamaa alimaanisha nin eti PHYSICS hataitumia sasa sijui hizo diode , transist , inductor , capacitor sijui zena diode laser diode ,transfoma atazipata wap
 
Wadau mimi ni kijana nilikimbia shule nikiwa form one but now naitaj kurudi school november 13th ila nitasoma QT na ndoto yangu ni kuwa Engineer wa electronics zote i mean computer na vifaa vinginevyo vinavyoendana na technology TV's phones consoles etc...

Wasomi ni wengi humu Jamiiforums please naomba ushauli nifuatilie masomo gani, ili nipate njia rahisi ya kutimiza ndoto yangu.

Natanguliza shukrani na mchango wenu ni muhimu kwangu

If I were to advice you kamwe nisingekwambia ukasome hizo Engineering kwa hapa Bongo bado bado kibishi...
Or less nambie hiyo Engineering unataka ukaisomee nje ya nchi

The only subject that will forever pay you is only Biology and this undebetable ofcourse

With Biology you are 95% confident that the gvt will employ you and 100% confident that you can employ yourself both inside the country and abroad...

Watu wanasema "Education for self employment" lkn hii ni changamoto kubwa hapa kwetu amini usiamini ndo maana wengi wakisikia issue za ajira wanazikimbilia na isitoshe kuna engineering hunaweza usiweze kabisa kujiajiri kulingana na capital inayoitajika...

Najua fika unaenda shule karibuni lkn mm naimani bado unayo nafasi kama unauwezo Shikiria BIOLOGY utarudi hapa JF kunishukuru baada ya miaka kadhaa
Najua unajisemea moyoni hauwezi lkn ushauri wa bure shikiria hizo Physics na Maths ila usisahau Biology na Chemistry

Mwisho,nikuombe samahani kwa kuja na story tofauti
 
Ndiyo maana nimeomba ushauri ata hivo ninajisikia free kusomea engineering bcoz napenda sana nijihusishe na technologia
 
Ndiyo maana nimeomba ushauri ata hivo ninajisikia free kusomea engineering bcoz napenda sana nijihusishe na technologia

Yes uko sahihi na hamna Technolojia inayolipa kuzidi Genetic Engineering ambayo hauwezi kuisoma kama haujasoma Biolojia,Usije ukafikiri technolojia imeishia physics na maths tu
na usifikiri huko chuo kuna vitu extra ordinary ni blah blah nyingi,Ndo maana nikasema Tanzania Engineering ni kazi bure tender zote wanakula Makaburu,wachina na ngozi kama hizo
tena kama unataka technolojia ziko VETA ndo maana unawaona watu kama Transistor humu JF kila siku wanakuja na thread ya ugunduzi wa Circuit ya kukamata wezi na circuit za security nyinginezo
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu mkuu yaan nimefikiria huyu jamaa alimaanisha nin eti PHYSICS hataitumia sasa sijui hizo diode , transist , inductor , capacitor sijui zena diode laser diode ,transfoma atazipata wap

Hakusema anataka kua engeneer wa umeme,amesema engeneer wa mambo ya computer,eletronics na mambo yote ya technology....
 
Sio engeneering zote zinahusisha physics,mfano software engeneering.

Wewe wasema kijana...ila wanaoijua fani ya uhandisi pasi na shaka wapo kimya

Btw mleta mada ana mpango wa kufanya Electronics na sio Software...
 
Genetic engineering haiitaji uwe na hivo vipindi priority ni Biology na chemistry

Au nayo hiyo sio engineering?

duh!!!

mkuu naomba ufanye kugugo utapata majibu mazuri zaidi...

ila naomba majibu yangu yasomwe kulingana na muktadha wa mleta mada....
 
Btw mleta mada ana mpango wa kufanya Electronics na sio Software...

Hakusema hilo specifically kama ulivyoandika. Amesema electronics,computer,simu na mambo yote ya technology. Kwa hiyo ana chaguzi nyingi au mawazo mengi kuhusiana na hayo mambo maana hawezi kusoma yote kwa pamoja lazima atachambua mahususi kwake.

Kama ndio hivyo ulivyoandika physics hataiacha maana atakutana na mambo ya circuits ambazo ni ufaham wa physics.

Btw nilichokisema awali haikua uongo,inategemea yeye anataka kufanya nini specifically. Yeye ameomba ushauri general,jibu langu lilikua mahala pake.

Asubuhi njema.
 
Back
Top Bottom