Acha kuandika mambo usiyoyaelewa wewe na kuleta copy & paste vya hapa na pale!
Hivi unafahamu ya kwamba oil inauzwa kwa dola ya Marekani?
Na hii ni Dunia nzima kila nchi inayonunua Mafuta ni lazima walipe kwa dola na hii ni kuanzia Albania mpaka Zimbabwe na kila lita ya Mafuta inayouzwa Dunia hii asilimia fulani lazima iende Serikali ya Marekani!
Unafahamu ya kwamba kila Dola moja inayaotumiwa Dunia hii ni lazima sehemu ya asilimia yake iende Marekani?
Hakuna Kampuni Dunia hii yenye fedha ama thamani klk Serikali ya Marekani!
sasa 150 bilioni Dola wewe ndio umeona ni fedha nyingi kuliko Serikali ya Marekani?
Bajeti ya Jeshi la Marekani peke yake ni zaidi ya Dola bilioni 500 na hicho ni kitengo kimoja tu, sijaongelea Elimu kwenye mambo ya Utafiti (R&D), miundombinu, Mishahara ya Wafanyakazi n.k
Marekani wana Military base Dunia nzima kuanzia Okinawa Japani mpaka Africom, Stuttgart Ujerumani na huko kote wamewekeza hela ndefu wewe unakuja kuongelea eti dola bilioni 150, hicho ni kitu gani?
Acha kudanganyika Serikali ya Marekani inauwezo wa kuchapisha hela kupitia FED na wanafanya hivyo kila siku, hivyo Apple hawawezi kuwa na fedha nyingi kuizidi Serikali ya Marekani!!
hapo kwenye red nimecheka sana, kaka inaonekana mnaongea maneno yenu ya mtaani na mnalishana sumu, hujui kama serikali ya marekani ikiprint hela nyingi na nchi nayo itaathirika kiuchumi?
hivi hujawahi kujiuliza kwanini serikali ya tanzania isiprint hela nyingi kila mtu akapewa chake wote tukawa matajiri? jinsi unavyoprint hela nyingi na ikaingia kwenye mzunguko ndio jinsi unavyomaliza uchumi nitakuelezea kimifano zaidi.
serikali ya tanzania imeprint hela kibao na imenunua na kufinance mambo mengi, hela zote zimekuja mikononi mwa wananchi mimi mkwawa na watanzania wenzangu kila mmoja ana mamilioni ya hela, kuanzia leo sitaki tena kutembea kwa miguu na mimi nataka gari, hivyo naondoka na milioni zangu kadhaa naenda show room ya magari. kufika show room nakutana na watanzania kibao sababu kila mmoja ana hela za kutosha yule mwenye show room kwa sababu anaona kuna wateja wengi anaamua kupandisha bei sababu bidhaa yake imekua adimu kibajaji tu kinaanzia milioni 60. hali imekuwa tata inabidi magari yaletwe mengi lakini uwezo wa kiwanda kuzalisha ni ule ule hivyo inabidi mashine na wafanyakazi watumie muda wa ziada kuzalisha, jinsi wanavyotumia muda mwingi kuzalisha ndio wafanyakazi wanavyodai mishahara mikubwa, bandarini nako misongamano ya bidhaa mikubwa wafanyakazi nao watadai nyongeza ya mishahara hali itaendelea hivi hivi kila mtu ataenda tibiwa hospitali za private hivyo hospitali watapandisha bei sababu watu ni wengi mwisho wa siku inflation kubwa inatokea na nchi inaathirika kiuchumi.
hope umeelewa hapo
tuje kwenye serikali ya marekani vs apple
inaonekana kaka hata maana ya cash hujui ni nini chukulia mfano huu
mfanyakazi A
analipwa shilingi milioni 8
-ada ya watoto analipa milioni 2
-matumizi ya nyumbani milioni 4
-kodi ya nyumba milioni 1 na nusu
hivyo kwenye mshahara anabakia na laki 5 ya matumizi
mfanyakazi B
analipwa shilingi milioni 2
-ada ya mtoto anasoma st kayumba shilingi 10,000 tu
-matumizi ya nyumbani 690,000
-kodi ya nyumba laki 3
mwisho anabakiwa na milioni 1
mfanyakazi A japo anaingiza hela nyingi ana cash kidogo kuliko mfanyakazi B
unapozungumzia cash ni kile kiasi cha hela ambacho kipo ready kutumika, sasa hela zishaenda kwenye defence budget inamaana si za serikali tena ni za wanajeshi, na hata apple akimchallenge marekani tujenge jengo refu lenye thamani ya dola bilioni 100 serikali haiwezi ku afford sababu haina cash hela zote zimetumika na matumizi yake makubwa
hope na hapo umeelewa