Nissan Dualis Imetembea Non Stop Dar to Musoma

Hata mi naelewa hivi.

Engine za gari zimesukwa kitaalamu kiasi kwamba kama zinafanya vizuri basi hakuna haja ya kuogopa kitu.
 
Acha genye
Anawashwa kijambio huyu
nyie machocco tu, watu wanasafiri na pikipiki boxer mtwara to morogoro non stop itakuwa gari yenye cooling system ya uhakika? au ndo mawazo yenu ya kimaskini, kuna mabasi yanasafiri dar to mwanza na yakifikia asubuhi yanageuka tena daily
 
Wakuu zangu nimetembea na Nissan Dualis Mpaka Musoma pasipo kupumzika na kuizima.

Je, vipi kuhusu Gearbox yake kwa Skendo za kufa? Kweli imenifurahisha na imetembea sana.
Mkuu, usijali wala usikhofu, hao wanao kutisha wanazifananisha hizi nissan kuwa kama toyota.
Jameni, msichukue mawazo yenu ya Toyota mkatuletea kwenye Nissan.
Nissan sio Toyota.
 
Mzee faini za tochi ilipiga mara ngapi ila pole na safari kama gari hikuripuka moto hongera.......
Hii Chuma ni shidaa...
Inavuta mpaka nachuana na Gari za Serikali
 
Wape elimu vijana...
Maana ukisoma koment za wengi humu utagundua hawajui chochote kuhusu magari....
 
Aisee..
 
yani hata cruser hard top siwezi ifanyia ujinga kama huo asee, panda nyeunge moro mwanza kashukire kituoni buzuruga uone nzigo unavo pozwa, sasa hako kakiberi nakushauri kauzie huko huko
Hii Gari anatak kuiua mapema mno
 
Wakuu zangu nimetembea na Nissan Dualis Mpaka Musoma pasipo kupumzika na kuizima.

Je, vipi kuhusu Gearbox yake kwa Skendo za kufa? Kweli imenifurahisha na imetembea sana.

Kamwe usiwaamini mafundi, huo ndo ushauri, google kuthibitisha maneno yao, mafundi wa dar ni wa hovyo, wezi, walaghai, wahuni na washenzy.
 
Hakuna gari ambayo haiwezi kufanya hivyo.itategemea uimara wake ukoje na service umefanya ya kiwango gani kabla ya safari.
Ni vema kuipumzisha Kila Baada yakilometa kadhaa, Naamini Kuna mahali ulikula au kujinyosha na kuchimba dawa
 
Wakuu zangu nimetembea na Nissan Dualis Mpaka Musoma pasipo kupumzika na kuizima.

Je, vipi kuhusu Gearbox yake kwa Skendo za kufa? Kweli imenifurahisha na imetembea sana.
Haina shida boss mie nmeshawahi kutoka nayo from mtwara to mwanza kupitia dar bila kuiIma vile vile sababu msukuma yule alikuwa anataka j3 awe kazini.

Gari ilitoboa na mpaka leo jamaa anaitumia sema tu tulipiga service ya maana almost 2m kasoro ilizama tyre mpya kila kitu kilikuwa kma gar imetoka japan

Ugonjwa wa hizo gari ni pale utakapoanza kuweka spear na service za kunjunga ndo hpo lazma uje kulia.

Pia issue ya pili hakikisha likitokea tatizo la wiring/umeme wa gari basi mpe fundi maalum wa nissan syo hawa mafundi wetu wa mtaani anaekata nywaya toka huko na kuja kuunga bila kujua nywaya hii ya wapi na usifanye matengenezo ya umeme bila kupima na diagnosis mashine.

Kwani ukifanya kuripua tu kwenye wiring kwa fund wa chini ya mti sku ikitokea loose kidogo tu utashngaa tu gar uko ndan kwako nje inaungua au hata kwenye foleni chombo limelipuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…