Ni gari ngumu imara, lakini spare zake ni ghali sana.
Service ya kawaida haipungui 800k
Service kubwa inachezea 1,500k na kuendelea.
Gari za nissan tatizo pekee ni ughali wa spare..nimezitumia gari hizi na toleo la lililotangulia kwa takribani 12yrs
Haya si ya kweli ndugu.
Mimi ninazo Y61 mbili zenye engine ya TD42, moja pick up na nyingine Wagon. Nimeziendesha zaidi ya kilometa 140,000 kila moja. Ni magari magumu yasiyokuwa na shida. Yanafanana sana na Landcruiser 80 series zenye 1HZ. Ziko comfortable, hazina longo longo za umeme— ukiondoa taa, redio na honi. Zinavumilia sana, ukizingatia kwa matumizi yangu ya kilimo na kazi za uhandisi zinazonilazimu kusafiri masafa na maeneo yenye miundo mbinu mibovu.
Matumizi ya mafuta inategemea na uzito wa mguu wako wa kulia ila tarajia kati ya kilometa 6.5 mpaka 7.5 kwa lita. Hazipendi kulazimishwa kuchanganya wala kupanda milima kwa kasi, ukizibembeleza (usizidi 90km/hr kwenye gia ya tano) unaweza hata kupata kilometa 8 kwa lita, ingawa sijawahi kufanya hivi.
TD42 ni engine mechanical, asilia yake ni miaka ya 1980 hivyo usitegemee miujiza ila hazichagui oil wala diesel. Zina oil filter 2, bei ya filter original au zile za GUD ni 30,000 kwa moja. Mimi hubadilisha air filter/cleaner kila baada ya service 2, na bei ya original air filter ni 60,000-75,000. Oil zinaingia lita 10, unaweza kuweka oil ya kawaida au synthetic.
Matengenezo makubwa ni kwenye bush, tierods na suspension links. Hizi pia hutegemea ruti zako. Kwa ruti zangu mimi, hubadilisha hivi vitu kila miaka 2/3, au baada ya angalau kilometa 30,000 hivi. Hivi vikorokoro huwa ghali ila bei hazitofautiani na vifaa vya Cruiser.
Spea za Y61 zimejaa kila mahala, zinaingiliana na magari mengine yakiwemo Cruiser 80.
Nimeendesha HZJ79, VDJ76, HDJ 101 pamoja na 80 series nyingi, Y61 hazina tofauti kubwa na Cruiser. Ziko more comfortable kuliko Cruiser zote nilizotaja kasoro HDJ101 (kutokana na hii kuwa na wishbone mbele).