Nawaza tu, mchina ataweza kuwa na ubora wa kukaa miaka 20-30 road.. just imagine leo kuna mtu ananunua ist ya 2006, rav 4 ya 1999..
Road ni gari chache sana za ndani ya miaka 10, chache zaidi za ndani ya miaka mi5.
Mchina sina wasiwasi na battery, nina wasiwasi na components nyingine za gari. Yaani leo BYD Dolphin mpya $10,000 imagine ikikaa miaka mitano ndio tununue used, si itakua $2,000
Tesla ameweza kuvuka miaka 10, na bado yuko vizuri ingawa inashuka thamani zaidi ya 60% kwa bei ya mpya.
Ukinunua EV nunua ambayo utakaa nayo ata 5-10 years, na uiendeshe kwelikweli. Tuombee Mchina afikishe hivo
Mi uwa nafuatilia Japan amenunua EV kiasi gani. Tatizo Wajapan wana ushamba kama wa USA kuthamini vitu vya nchini kwao, na nchi ya JP kwenye EV wapo nyuma bado.
Kwanini nafuatilia JP, kwasababu Watanzania ndio tunaagiza magari toka uko wengi, kwahiyo yakiwa mengi, inamaana soon used zitakua nyingi, ambazo ni RHD, na soon zitashuka bei.
Optiom rahisi utoe South kwa bwana
Isanga family