Nissan X-Trail

Usihangaike na kutaguta CAT kwanza ni garama kubwa but huo ugonjwa una solution kama 3 hivi ninazo zifaham mimi..kuzidelet hizo oxygen senaor kwenye ECM control box, kuzifanyia utundu kwa kuidanganya control box hapo pia kuna njia mbili. Na mwisho kufunga kimodulatot..

Njia rahisi na yenye garama ndogo ni hiyo ya pili.kama utahitaji tuwasiliane mkuu nitakuelekeza jinsi ya kufanya..buree kabisaaaa
 
kuna ndugu yangu mmoja aliniambia kuwa aliambiwa na fundi magari mmoja kuwa magari YOTE ni pasua kichwa! ukijumlisha na jinsi wadau wanvyo yananga humu nilishaanza kuamini pia...japo nilikuwa nakilia timing ka Nissan Note ila wana jamvi wakanikata stimu kabisa!
 
Hapa uchambuzi wa kitaharam hadi raha issue ni kuwa kwa mazingira ya vijini hamna mafundi wa uhakika wataharam nauliza vipi engine za 2AZ vvt-i ufanisi wake na service zake pia zikoje? Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa uchambuzi wa kitaharam hadi raha issue ni kuwa kwa mazingira ya vijini hamna mafundi wa uhakika wataharam nauliza vipi engine za 2AZ vvt-i ufanisi wake na service zake pia zikoje? Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingawa huu ni uzi wa Nissan Xtrail, Toyota 2AZ VVTI IPO vizuri ila mafuta (oil) unayoitumia pale lazima iwe synthetic na ufaatilie vizuri change-interval/ubadilishe kw mda maalum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijakuelewa mkuu unaposwma oil na mafuta inabidi oil yaje je change interval ya km ngapi inafaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Engine oil inayofaa kw engine za kisasa ni ile ya SYNTHETIC(kw.mfn. Total Quartz 9000, Mobil1, Shell Ultra, n.k.). Change interval ni km elfu tisa hadi kumi au mwaka mmoja.
 
Engine oil inayofaa kw engine za kisasa ni ile ya SYNTHETIC(kw.mfn. Total Quartz 9000, Mobil1, Shell Ultra, n.k.). Change interval ni km elfu tisa hadi kumi au mwaka mmoja.
Mmm mbona labda nimeachwa km 9000 kwa service au
 
Hbr za mida WanaJF
Baada ya kuangaika hapa na pale, catalyctic converter ya Xtrail QR20DE tumeipata na kuifunga kwenye gari. Mngurumo na idle speed zilibadilika pale pale. Zile sensor zake (O2) pia zilionekana zikifanya kazi yake bila tatizo. Baada ya mda kidogo hata ile harufu kali ya mafuta kwenye exhaust iliisha na gari likawa tulivu.
La msingi ninalotarajia ni matumizi yake ya petroli kupungua. Hii inatokàna na utendakazi wa mifumo na sehemu husika za engine kurudi sawa.
Matunzo na marekebisho ya gari sio kama uganga, manual na maelekezo yapo.
 
Mkuu hebu tujuze hicho kifaa kimepatikana kwa bei gani na kufa kwake kulisababishwa na nini? Nategemea kununua hii gari miezi michache ijayo ndio maana nauliza.
 
Mkuu hebu tujuze hicho kifaa kimepatikana kwa bei gani na kufa kwake kulisababishwa na nini? Nategemea kununua hii gari miezi michache ijayo ndio maana nauliza.
Asante kwa swali zuri sana Bw. Galindas. CAT converter ni kifaa kinacho nasa gesi na chembechembe haribifu kwa mazingira na kuziangamiza kw kuzichoma na kuzichanganya zikawa safi(harmless). Mle ndani kuna madini yanayosaidia katika shughuli hii, na pia muundo wake ni maalum kunasa chembechembe zile na kuzipika kwa joto la juu.
Tukilinganisha mfumo huu na kichujio, kwa hii ndio mmoja ya kazi yake, tutaona kua kuna uwezekano wa mfumo kuziba. Engine ikichoma mafuta mengi kupita kiasi, moshi hasaa carbon uzidi na kuziba mfumo. Kuliwasha gari ukiwa umekanyaga mafuta au kulipa mafuta linapowaka ni mwiko kw magari yaliyo na mifumo hii.
Magari ya Xtrail yanatumia mifumo electronic ya mafuta na kwa hivyo tatizo kidogo laweza leta majanga. Mfano, taarifa kuhusu jiko(combustion) kutoka kwa oxygen sensor zikikosa, injector umwaga mafuta mengi na kuzidisha carbon.
Kwa sababu ya i) madini nadra yanayotumika kuzitengeneza mifumo ya CAT converter na DPF, ii) sheria kali za kulinda mazingira hasaa ulaya na nchi zilizoendelea na pia iii) soko la kununua CAT/DPF mbovu mbovu ili kuvuna yale madini, mifumo hii ina bei sana mpya au used. Ile ya Xtrail niliinunua laki nane!
 
Nimekuelewa sana mkuu. Nikupongeze kwa kazi nzuri. Endelea kutujuza hasa pale unapotatua shida mbalimbali za haya magari.
 
Mkuu uwe unaweka na mawasiliano kabisa ili watu wakupe kazi.
 
LEGE unapatikana wapi dar, huwa nafuatilia post zako vizuri sana, una ujuzi mkubwa na ufundi wa magari is what i can conclude.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…