Hbr za masiku WanaJF
Siku mingi sija changia uzi, mtanisamehe ila shughuli na kazi zinabana.
Leo nimeipata Xtrail ya petrol imesumbua kwa mda. 'Wasanii wameipigia show'; cat converter wameitoa matumbo, oxygen sensor wamebadilisha, head wameng'oa na mambo mengine mengi.
La kwanza kufanya pale ni kukagua 'vital parameters' kwa engine kama vile oili, air filter na kadhalika. Niligundua oili imechoka kweli na nyeusi sana - kumbuka gari lilikua kwa fundi siku tatu awali. Hili lilieleza mambo/observations flani nilipo liwasha gari. Engine Idle Speed ilikua juu na haijatulia; 900-970 rpm, exhaust ilinukia rich sana na mengine.
Diagnosis report ilitoa code zifatazo: P0172- fuel trim, too rich
P0120- throttle position sensor
P1123- ETC motor control circuit; mambo haya matatu yanahusu mfumo wa mafuta - fuel system. Observations zetu pale tulipoliwasha gari ziliashiria haya lakini bila kuyapata 'from the horses mouth' hakuna uhakika ila ni kukisia tu.
Bila kuongea mengi kuhusu ufundi au ujuzi wa mafundi, taratibu na itikadi za kiufundi ni muhimu kuzingatiwa. Mambo ya msingi kama kubadilisha oili na filter yana adhiri utendakazi wa engine na mifumo mingine. Ni wazi kwa kila mtu kua oili ulainisha vyuma na sehemu kwenye mfumo. Utelezi huu unahitajika kurahisisha mizunguko na kadhalika
Ubora/property hizi upotea oili inavyozeeka au inavyotumika kwenye mfumo - iwe engine, gearbox(manual au auto), diff, pump za hydraulic na pia compressors. Utapata unavyokaa na oili chafu kwenye mfumo, mfumo unapata uzito mkubwa na hapo kuhitaji nguvu zaidi kuendeleza mzunguko.
Zoezi la marekebisho kwa hili gari litaanzia na kuifanya engine service ndio tufanye tune-up ya mfumo wa mafuta. Ni muhimu kuelewa kua mifumo ya computer imewezeshwa kusoma, kusahihisha na pia kutarajia mabadiliko/mapungufu flani kwa ajili ya kuzeeka au mazingira.
Bila kujua hili, 'adaptation' za kawaida za mfumo zaweza chukuliwa kama matatizo na pale 'fundi' akaliharibu gari. Itaeleweka pia mambo haya yanafanyika kwa/na mitambo ya umeme. Mawasiliano yanategemea na kulingana na misingi flani ya kiufundi, kilele chake hua ni pale mtu anapotumia mfumo wa muunda gari - OEM, unaposhuka ngazi ndio mawasiliano yanavyokua ya kubahatisha.
Unapohisi gari/engine ina behave tofauti, ebu jiulize service iko due au kama ni baada yake, ni kipi kilichobadili kwa zoezi.
Pamoja!
Sent using
Jamii Forums mobile app