Naomba nikuambie kitu, japo najua wenye Toyota zao watakuja kupinga, siwakatazi kupinga kwa sababu kila mtu ana uhuru wake...
Sikushauri utoe thermal start kama watu wanavyokushauri....Mjapan aliyeiweka si mjinga.
Hizo habari za kwamba Xtrail zina ugonjwa wa kuchemsha ni MYTHS tu ambazo watu wamekuwa wakiamini kwa sababu..
Nissan xtrail huwa halitaki kuweka maji ya bombani kwenye radiator, wabongo tunapenda urahisi wa mambo...unakuta mtu anamiliki vitz anaweka maji ya bombani, basi na kwenye x ttail anafanya hivyo....x trail iwekee coolant iliyopendekezwa... coolant hupooza gari kwa kiwango kinachotakiwa tofauti na maji ya bomba, kisima au mtoni.
Weka engine oil iliyopendekezwa na mtengezaji sana sana iwe 5w 30...kibongo bongo tunaamini zaidi Castrol au Total.....kumbuka oil mbali na kulainisha injini, pia hupooza injini..
Mara kwa mara hakikisha kiwango chako cha coolant hakishuki below the minimum level.
Kuna watu wapo wanamiliki x trail zaidi ya miaka 6 sasa, wameshafanya nazo masafa karibu mikoa yote na nje ya nchi mfano Kenya, Uganda bila kufanya modifications zozote kwenye engine....
Ingekuwa haya magari ni mabovu kama watanzania wanavyosema, Nissan Motors Corporation Japan wangeshasitisha uzalishaji wake...ina maana ni gari zinazofanya vizuri ndiyo maana uzalishaji wake unaendelea na sasa Nissan Xtrail wapo Generation ya tatu kama sikosei...
Mafundi wa Tanzania hawataki kusoma, wamezoea mifumo ya Toyota, hivyo wao ndiyo chanzo kikubwa cha kuwakatisha watu tamaa kwa upande wa xtrail....
Sisi watanzania ni watu wa ajabu..mtu akishindwa kitu hataki kukubali, anakiponda...mafundi wengi x trail zinawatoa jasho, kwa hiyo wanawadanganya watu hizi gari hazitengenezeki....
Kwa ninj zisitengenezeke, gari lina OBD, ni kiasi cha kusoma code na kuitafsiri inaashiria nini, then you do a replacement
Chonde chonde, x teail usiipeleke kwa mafundi makanjanja, mwembeni...ukihisi tatizo weka vipimo vya computer, replace parts with genuine ones......hapo x trail utaiendesha miaka 8 bila kujuta.
Siku zote usichukue experience ya utunzaji wa Toyota ukaihamiahia kwenye X trail..hapo utateseka...
Mwisho.....gari ni matunzo kwa kuzingatia instruction manul yake.....na si kwa kuzingatia maneno ya watanzania.