Nissan XTrail hii ina tatizo gani?

Nissan XTrail hii ina tatizo gani?

Wakuu habarini

Wajuzi na wataalamu wa hizi gari naomba kujua tatizo la hii gari yangu yaweza huwa nini? Huwa inajiweka free yenyewe ikiwa kwenye mwendo, inakuwa kama inasleep na wakati huo ipo kwenye D. Na nilichojaribu kwa utundu nimejaribu kuiweka N ikiwa kwenye mwendo nikaizima na kuiwasha juu kwa juu kurudisha D inakubali kupokea mwendo, msaada wakuu
Mungu wangu usijaribu huo mchezo tena! Hilo tatizo angalia kiwango cha hydraulic na zingatia aina ya hydraulic iliyopendekezwa! Nissan zina hydraulic yake special

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni speed sensor ya kubadilisha tuu. ni sensor ndogo inakaa ubavuni mwa gear box. Hili ni moja ya ugonjwa wa magari mengi ya Nissan.
 
Back
Top Bottom