Nissan xtrail inanitesa.

madabadaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
288
Reaction score
178
Heshima kwenu wakuu.

Niko na shida sana nahitaji msaada wenu hili gari lina mauza uza balaa.

Nikiwa njiani kuelekea kazini nilistukia ghafula gari linaunguruma tu nikikanyaga moto linaunguruma tu hata halitembei, hivi sasa nimelipaki kwa kulisukuma pembeni mwa barabara nikisaidiwa na wasamaria wema.

Hii ni Mara ya nne hili gari kufanya hivi safarini na kila Mara lilipofanya hivi lilirudi ktk hali ya kawaida bila ya kufanyiwa matengenezo maana hata fundi wangu huchemka kwa kutobaini chanzo cha tatizo.


Walio na ujuzi naombeni ushauri wenu nini tatizo la hii nissan xtrail maana fundi wangu hajabaini chochote.

Nawasilisha.
 
Hiyo check air flow meter, au njia za upepo, njia ya fundi wako kujua ni kuwasha gar anapuliza spray kwenye kila maunganusho ataona ni wapi inavujisha upepo kwenye engine, nadhan ni hilo niliwahi ona garage gar ilokuwa na shida hiyo ikirekebishwa kwa vitu hivyo viwil.
 
Wapelekee mafundi wa Nissan katika garage zao
 
Nahisi tatizo ni quality ya service unayofanyia gari lako
 
Nadhani tatizo kubwa hapo sio gari, ni hao mafundi wako unaokiri mwenyewe kuwa wanachemsha na hawajui cha kufanya. Gari hizi hazitaki longolongo kwenye ufundi. Engine zake QR20 na MR20 hazitaki mafundi vilaza.
Xtrail ni gari nzuri sana ina balance sana barabarani na huko kwenye vumbi na tope inapiga mguu kwa mguu na landcruiser.
Nimzeitumia miaka mingi.
 
Mafundi walio specialize kwenye Nissan nawapata wapi? Je naweza pata contact zao? Mie nahisi nimeunguza plates za clutch. Haibadili gear.
 
Hiyo ni gear box itakuwa imeaga dunia
 
Service yako mbovu Mkuu... Hizo gari zina vitu vyake special..... Tafuta mafundi wa Nissan
 
Kama upo Dar, kuna fundi mmoja anaitwa Hassani. Alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Nissan lakini alikuwa anafanya kazi zake jioni au weekend kule mabibo kwenye garage yake.

Mtafute kama upo Dar, japo ana bei kidogo lakini anajua anachokifanya. 0755 109 405, 0717 441 096. Ukiongea naye msisitizie yeye ndiyo afanye ufundi na sio vijana wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…