Nahitaji kununua xtrail 2003 yenye engine ya SR20VET,
Nanunua modeli yenye engine ya SR20 kwa sababu engine hiyo inasifika kwa uimara duniani kote na ni nyepesi kwa mafundi kuirekebisha endapo ikisumbua.
Kwa wale waliowahi kumiliki xtraili hasa ile yenye engine ya 2.0L au cc 2,000 naombeni mnipe uzoefu wenu. Hii gari inakunywaje mafuta ? Binafsi Ningependelea nipate angalau 11km/L au nitembee kilometer 11 kwa kila Lita moja.
Mkuu sikiliza nikupe fact kidogo juu ya xtrail as namiliki hili gari huu mwaka wa nne na niliitoa japan, itapendeza kama mtu ambaye hajawahi kumiliki gari za nissan au hata kuendesha gari ya above 1500cc aache ku comment as you have no idea rather mnapotosha.
Kwanza niseme wazi gari za nissan as for Benz BMW range etc hazihitaji mtu mwenye kipato cha mawazo au anayetegemea kuuza baada ya siku chache.This is about purchasingbpower and affordability.
Gari hizi hazihitaji mafundi wa kuunga unga na spea za kufananisha au kufitishia rather genuine spare parts.
Mfano extrail uliyotaja inatumia gear box oil ya fuild matic J ambayo lita moja inauzwa 50,000 ipo kisangani auto ,master cad auto wako msimbazi dar au authorised dealers wa nissan na gari hiyo itahitaji lita 4.
Engine oil inaweza kuwa synthetic au ya kawaida mfano BP standard lita 5 inafika hadi 55,000 ila unatumia lita 4.
Brake.pads mfano zile genuine za mbele ni 220,000.
Hio ni baadhi ya mifano tu ila my point is hizi gari zisizotaka mafundi kanjanja na spea za magumashi.
Juu ya fuel consumption hiyo yako ya 2003 unaweza kwenda hadi 1l/11km with full ac..mimi iko hivyo as ni la.muda na all the time natumia ac hata iwe arusha.
Well,ni gar za kueleweka ila waliozoea vitz starlet etc na ambao wana limited understanding plus kipato cha mawazo watakuambia ni ndoa ya kikristo.
Just ishi ndoto zako as far as you can afford.
Karibu kwenye team ya xtrail!