Nissan xtrail inatumia mafuta kiasi gani kwa uzoefu wako

Nissan xtrail inatumia mafuta kiasi gani kwa uzoefu wako

Kwa ujumla hii Gari ni nzuri sana na huwa haziharibiki ovyo ovyo.

Niliwahi kuendesha moja kwa km 120 bila engine oil bila kujua lakini nikafika bila tatizo. Nilivyogundua nilitamani kulia
 
Umefafanua vizuri sanaa. Naomba kujua hiyo engine oil inachukua kilometer ngapi kubadili ukiweza tupe na kilometer za transmission fluid.

shukrani.
Engine oil mara nyingi ni km 3000 hiyo bp standard ..ila ukinunua pure synthentic kuna za mpaka km 10000
.ila kama una uwezo haishauriwi ukawie kumwaga oil chafu as unaua gari..pia ubadili oil filter.

Hiyo fluid matic J unaweza piga hata km 100000 kwa maana ingine gear box oil haitakiwi uchokonoe chokonoe.
 
Ni Post ya zamani lakini sababu na mimi natumia hiyo gari naomba nichangie,ninamiliki xtrail Zaidi ya mwaka wa tano sasa,nimewahi kumiliki Rav 4 na xtaril kwa wakati mmoja,niliuza Rav 4 nikaamua kubaki na Xtrail sababu ni kuwa moja Xtrail iko comfortable Zaidi na spacious kuliko Rav 4 lakini pili ilikuwa rahisi kuuza Rav 4 kwa sababu watu wanazipenda kwa kuwa ni rahisi kui maintain.
Nilinunua Xtrail ikiwa tayari imetumika hapa nchini na wachina waliokuwa wanajenga barabara so haikuwa vizuri sana ukilinganisha na kipindi unaagiza Japan,baada kama ya mwaka mmoja ,nilibadilisha Engine,baada ya gari kuanza kuchemsha,tatizo lililosababishwa na cylinder head na chanzo nafikiri ilikuwa na radiator.baada ya kubadlisha cylinderhead gasket mara mbili na kupiga pasi cylinder head niliamua kubadilisha engine.
Nikiri kuwa toka nibadilishe Engine na cylinderhead sikuwahi hata kuongeza maji Zaidi ya top up ya kawaida gari ikienda Garage,Nimesafiri na hiyo Gari karibu Tanzania nzima,kuanzia Kigoma,Kagera,Katavi ,Mbeya na haikuwahi kunisumbua.
Matatizo common ya xtrail kama yanavoripotiwa na mafundi mara nyingi ni Gearbox,Exhaust System pamoja na engine kama nilivoelezea hapo juu.
Sijawahi jutia kumiliki xtrail na ikitokea siku nikauza hii xtrail,hakina Gari ntakayoagiza tena itakuwa ni Xtrail.
 
Mtaalamu wako ni muongo. Nissan zote, iwe Murano, Civilian, Rasheen Patrol, March, Condor ama Safari hazitaki service za mwembeni za kiubabaishaji. Mafundi wetu si wazoefu wa magari haya. Nissan wana oil zao na hydraulic fluid za gearbox special kwa magari yao. Ukitumia oil za multipurpose kama zinazotumika kwa magari ya toyota (dumu la lita 4 linauzwa shilingi elfu 28 mpaka 30) lazima gari ikuzingue na utaichukia. Hydrauloc fluid ya Nissan kwa kariakoo inaanzia 120,000/- kwa dumu la lita 4. Pili, nissan hawana spea nyingi feki. Hii ina maana spea zao sokoni ni ghali kwa kuwa no genuine, ndio sababu watu wanasema ni pasua kichwa. Lakini vinginevyo nissan ni gari ya kumiliki kama huna pesa za mawazo!
Hiyo hydraulic fluid kumbe nimepigwa?....asee!

Kutuma tuma huku![emoji15] [emoji15]
 
Anauliza ulaji wa mafuta wewe unajibu hataweza kuiuza!!!

Kifupi ni kuwa, hakuna gari mbovu au pasua kichwa. Shida ni kununua gari kisha mtu hufuati masharti ya utunzaji (maintenance) ya hilo gari. Na ugonjwa huu umeletwa na waliozoea Toyota maana fake spares nyingi na cheap. Sasa ukihamishia mazoea hayo kwa Nissan lazima uone ni “mbovu” au “pasua kichwa”.

Nissan ni gari imara na zinavumilia sana ubovu wa barabara zetu. Ila peleka service kwa mafundi wenye ujuzi na vifaa. Tumia oil genuine ambayo ni obvious haitakuwa cheap. Weka spare kwa wakati. Kama kuna part inahitaji replacement, “usivute muda” kwa vile iliyopo bado “ina nguvu”. Wrong!

Mwisho epuka “cheap” stuff.

Kwa ulaji wa mafuta wastani ni 8KM/L highway na 7KM/L urban tarmac road, 6KM/L rough road.
Hiyo replacement ya spare kwa muda muafaka ndo wabongo wengi tunazingua!

Na mara nyingi ikianza kuzingua usipobadilisha at time ujue unaharibu kwingine! Labda upaki
 
Mkuu sikiliza nikupe fact kidogo juu ya xtrail as namiliki hili gari huu mwaka wa nne na niliitoa japan, itapendeza kama mtu ambaye hajawahi kumiliki gari za nissan au hata kuendesha gari ya above 1500cc aache ku comment as you have no idea rather mnapotosha.

Kwanza niseme wazi gari za nissan as for Benz BMW range etc hazihitaji mtu mwenye kipato cha mawazo au anayetegemea kuuza baada ya siku chache.This is about purchasingbpower and affordability.

Gari hizi hazihitaji mafundi wa kuunga unga na spea za kufananisha au kufitishia rather genuine spare parts.

Mfano extrail uliyotaja inatumia gear box oil ya fuild matic J ambayo lita moja inauzwa 50,000 ipo kisangani auto ,master cad auto wako msimbazi dar au authorised dealers wa nissan na gari hiyo itahitaji lita 4.

Engine oil inaweza kuwa synthetic au ya kawaida mfano BP standard lita 5 inafika hadi 55,000 ila unatumia lita 4.

Brake.pads mfano zile genuine za mbele ni 220,000.

Hio ni baadhi ya mifano tu ila my point is hizi gari zisizotaka mafundi kanjanja na spea za magumashi.

Juu ya fuel consumption hiyo yako ya 2003 unaweza kwenda hadi 1l/11km with full ac..mimi iko hivyo as ni la.muda na all the time natumia ac hata iwe arusha.

Well,ni gar za kueleweka ila waliozoea vitz starlet etc na ambao wana limited understanding plus kipato cha mawazo watakuambia ni ndoa ya kikristo.

Just ishi ndoto zako as far as you can afford.

Karibu kwenye team ya xtrail!
Umemaliza chief[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Inaweza ikawa inatumia kama hii labda...[emoji30][emoji30][emoji30]
tapatalk_1521144929388.jpeg
 
Umefafanua vizuri sanaa. Naomba kujua hiyo engine oil inachukua kilometer ngapi kubadili ukiweza tupe na kilometer za transmission fluid.

shukrani.
Mimi ninatumia Extrail ya 2005, cc 1900. Nilianza kutumia hydraulic ya MATIC kama ilivyoandikwa kwenye stick yake,nilikuwa nainunua lita moja 50,000 pale Victoria Petrol Station, Kona ya JET(Nyerere Road) baadae nikampata mtu mmoja ameitumia gari hiyo muda mrefu akaniambia naweza kutumia Hydraulic inaitwa Atlantic, toka UAE. Inapatikana kwenye gallons fulani za bati. Bei yake ni between !20,000- 140,000 per 4 litres. Hiyo inakwenda km 9,000.
Engine oil natumua BP Synthetic last time nimeinunua kwa 60,000.00(five litres) pale Puma External. Ila inatumia lita nne hivyo unabakiza lita moja. Hiyo inatembea km 3,000 ndio unafanya service. Maana yake ni kwamba kila sevice tatu za engine ndio unafanya service ya gear box. (3:1). Siku unafanya full service angalau uwe na laki mbili mfukoni. Mambo mengine ni kawaida, mafuta inakula angalau 9-10 km/litre.
 
Mimi ninatumia Extrail ya 2005, cc 1900. Nilianza kutumia hydraulic ya MATIC kama ilivyoandikwa kwenye stick yake,nilikuwa nainunua lita moja 50,000 pale Victoria Petrol Station, Kona ya JET(Nyerere Road) baadae nikampata mtu mmoja ameitumia gari hiyo muda mrefu akaniambia naweza kutumia Hydraulic inaitwa Atlantic, toka UAE. Inapatikana kwenye gallons fulani za bati. Bei yake ni between !20,000- 140,000 per 4 litres. Hiyo inakwenda km 9,000.
Engine oil natumua BP Synthetic last time nimeinunua kwa 60,000.00(five litres) pale Puma External. Ila inatumia lita nne hivyo unabakiza lita moja. Hiyo inatembea km 3,000 ndio unafanya service. Maana yake ni kwamba kila sevice tatu za engine ndio unafanya service ya gear box. (3:1). Siku unafanya full service angalau uwe na laki mbili mfukoni. Mambo mengine ni kawaida, mafuta inakula angalau 9-10 km/litre.

Sio ghali, cha mwisho na naomba niulize kizungu maana sijui kwa kiswahili niwekeje.

Is it reliable and built to last?

Ahsante kwa mara nyingine.
 
Sio ghali, cha mwisho na naomba niulize kizungu maana sijui kwa kiswahili niwekeje.

Is it reliable and built to last?

Ahsante kwa mara nyingine.
My view,it is reliable and built to last if you adhere to its requirements. Timely services and genuine spare parts to mention a few. There is a common notion among people that its spares are rare and expensive, what I really don't buy.The spare parts are abundant these days and the price is reasonable. If your budget ranges between 12-14M, I would advise you to go for that. You won't be disappointed.
 
Back
Top Bottom