Nisubiri kwa muda gani ili kubeba mimba nyingine?

Nisubiri kwa muda gani ili kubeba mimba nyingine?

Ximena

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
641
Reaction score
353
Habari zenu,
Naomba mnisaidie kwa hili ingawa linaweza kuwa lishaulizwa lakini mimi ni mgeni humu. Hivi karibuni nilijifungua kwa operation lakini mtoto akafariki, nahitaji kujua ni baada ya muda gani itakuwa sahihi na salama kubeba mimba nyingine.
 
pole sana mdau. mi nasikiga ni baada ya miaka 3 ila tusubiri wataalamu watatuambia
 
Kwa mama aliyejifungua vyovyote vile. Wanashauri zipite angalau week sita. Sasa wewe unaweza kuangalia kuanzia hizo week sita kwenda mbele.
Halafu suala la kubeba mimba huwezi ukalipangia kihivyo kwa kuwa kuna vitu vingi vinahusika hapo. Mungu akipenda na kwa wakati muafaka atakupatia haja yako.
 
Inategemea na hali yako kiafya, umri na sababu za kufanyiwa operation kwa huo ujauzito uliopita maana inaanza miezi 6 , miezi 9, miez18. au baada ya miezi 23.ukionana na dk atafanya uchunguzi(hasa physical general assesment) na kujua sababu za hiyo operation ya kwanza atakushauri kitaalamu na mda mzuri..be serious uende kupata hiyo huduma kwa watalam usiulizee mtu asiyejua..ni rahisi sana kuja kupata complications tena
 
pole mpendwa!,inashauriwa ipite miaka mitatu....
Mmmh..its not rule of thumb..inategemea mambo mengi cha kwanza kabisa umri mtu wa zaid ya miaka 30 anaweaza kukaa zaidi ya miezi 24 lkn mf mtu wa miaka 25 anaweza kukaa miezi 9 tu..ukiweka na other conditions ziwe sawa
 
ahsanteni, umri wangu ni miaka 25 na ilibidi kufanyiwa operation baada ya mtoto kuonekana mkubwa na njia kutofunguka vizuri.
 
ahsanteni, umri wangu ni miaka 25 na ilibidi kufanyiwa operation baada ya mtoto kuonekana mkubwa na njia kutofunguka vizuri.
Kwa miaka 25 na kwa hiyo sababu ya kuwa na big baby unaweza kukaa miezi 6 mpk 9..kwa kuwa pia hunyonyeshi..lkn kwa nini mtoto alifafiki..? Ulikuwa na prolonged labor( muda wa kukaa labour ulikua mrefu sana zaidi ya masaa 18).?
 
ndio nilikaa zaidi ya masaa hayo nikiwa hospital hadi mtoto akaacha kucheza ndipo nilipopelekwa ultra sound wakasema amefia tumboni
 
Pole sana, kaongee na daktari aliyekufanyia C-section, ila ni vizuri kusubiri kwa miezi sita lakini muone Dr kwa ushauri wa kitaalam.
 
Pole sana, kaongee na daktari aliyekufanyia C-section, ila ni vizuri kusubiri kwa miezi sita lakini muone Dr kwa ushauri wa kitaalam.
ahsante, ila kuna umuhimu wowote wa kuonana na dr huyo huyo? maana to be honest i dont want to set my foot in that hospital again.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapana hakuna umuhimu huo, Dr yeyote mwenye uzoefu wa hali ya juu katika mambo ya uzazi na pia ana reputation nzuri kutoka kwa akina mama aliowahi kuwasaidia anaweza kukusaidia kwenye hili.

ahsante, ila kuna umuhimu wowote wa kuonana na dr huyo huyo? maana to be honest i dont want to set my foot in that hospital again.
 
ndio nilikaa zaidi ya masaa hayo nikiwa hospital hadi mtoto akaacha kucheza ndipo nilipopelekwa ultra sound wakasema amefia tumboni
Pole sana...kama ilikua hivyo unaweza kukaa kati ya miezi 18 mpk 23..ni lkn ni vzr ukipata nafasi uende hospitali zinazoeleweka kwa clinical assessment zaid...daktari ataangalia aina ya mshono..na afya yako kwa ujumla...lakini km ulikaa zaidi ya massa 18 na mtoto akafia tumboni muda sahihi ndo huo.. na kwa kuwa bado una umri mdogo ingekuwa unakimbilia 30 ingekuwa shida .pole sana mamy
 
Kwa miaka 25 na kwa hiyo sababu ya kuwa na big baby unaweza kukaa miezi 6 mpk 9..kwa kuwa pia hunyonyeshi..lkn kwa nini mtoto alifafiki..? Ulikuwa na prolonged labor( muda wa kukaa labour ulikua mrefu sana zaidi ya masaa 18).?
nashukuru kwa ushauri
 
Pole sana dada yetu. Insha-Allah mambo yatakaa sawa.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom