Nitaenda Kanisani kutoa sadaka maalum ya shukrani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Mungu Baba mwenye enzi yote Muumba wa mbingu na nchi asante baba kwa kutuvusha salama sisi CHADEMA kwenye huu uchaguzi wa kihistoria.

Mara tu baada ya ushindi wa Lissu nikajiwa na wazo la kurudi Kilingeni nikafanye kafara lakini nikakumbuka kumbe nilishatoka huko πŸ’ͺπŸΏπŸ™πŸΏ

Bila kusema uongo mimi ni mmojawapo wa wana CHADEMA walioumizwa vibaya sana na yale yote mabaya yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chama chetu.

Nikiri wazi kama ni kusali kuiombea CHADEMA basi kipindi hiki nilisali
. Mambo ya kuwatusi viongozi wakuu
. Mambo ya kuwadhihaki
. Mambo ya kuoneshana chuki za waziwazi kati ya makada
. Mambo ya kuzushiwa kila aina ya baya
. Post potofu zilizojaa uzushi na upuuzi wa kila aina hapa JF.. Na mengine mengi ni vitu ambavyo nilivibeba kwa maumivu makubwa mno

Kuna baadhi ya taarifa nilikuwa nazipata kutoka mbali jinsi mambo yanavyoendelea kuelekea uchaguzi wa kihistoria..zilikuwa zinatisha sana

LAKINI Mungu wetu ni Mungu wa wote na matendo yake si matendo ya binadamu.. Ametufuta machozi

Chama kilikuwa kinatengenezewa zengwe la mpasuko mkubwa sana.. In fact wangefanikiwa ndio ingekuwa mwisho wa CHADEMA😭😭😭

Sijui tungeenda wapi huko Mungu wangu.. Lakini kwa upendo wake mkuu Mungu wetu ametuvusha salama.. Hili nalo limepita.. Hakuna tufani nyingine itaweza kuitikisa CHADEMA kwa miaka mingi ijayoπŸ’ͺπŸΏπŸ™πŸΏ

Leo kwa mara ya kwanza ndani ya siku 30 nimehisi njaa na kula chakula amabcho naona kina ladhaβ€πŸ™πŸΏ

Nitaenda kutoa sadaka ya shukrani.
 
Yule mungu MUKU mungu wa Robert Herlieli Mtibeli
 
Kila lenye kheri, hongera kwa uaminifu na Shukrani kwa Mungu wako.
 
Amina, na ikawe heri zaidi Mtumishi!

Nahisi kulikuwa na maombi mengi na upatanisho wa watumishi wengine wengi wa Mungu, na wengine mpaka wakaanza kupaaziwa kashfa nyingi kipindi cha kampeni!
 
Hiyo hela tafuta watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu uwape!
Au tafuta hata mtoto wa shule umnunulie sare za shule au daftari.

Hilo litakuwa wazo bora sana kuliko kuwapelekea wanaojiweza huko kanisani na hawatakuwa na kumbukumbu yoyote juu yako.

Ni maoni yangu tu mkuu unaweza kuyapuuza ukiona inafaa kufanya hivyo
 
Sisali makanisha ya makanjanja.. Na kanisani kwetu tuna utaratibu wa matendo ya imani ambapo huwasaidia wahitaji mbalimbali kwenye jamiiπŸ™πŸΏ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…