G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Nitaenda kwa Mbowe ndani ya siku mbili hizi kumshauri asifanye dhambi kutufanya wafuasi wake tukafarakana kwa kipindi hiki muhimu kuliko nyakati zozote zile. Nitamsihi kuiona mbele ya CHADEMA.
Mimi nikiri wazi kuwa nimehuzunishwa sana na mambo ambayo baadhi ya wafuasi wa Mbowe ambao kiukweli siyo wafuasi wake bali wafuasi wa matumbo yao jinsi wanavyouchukulia uchaguzi wa chama mwaka huu.
Nimehuzunishwa sana na jinsi wanavyouchukulia uchaguzi wa CHADEMA ngazi ya taifa kwa kipindi hiki nyeti sana na aina ya siasa ambazo wenzetu CCM wamezifanya kwa miaka sita sasa.
Mbowe amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 sasa, amekiongoza chama vizuri katika nyakati zake na kweli tumekuwa tukimuunga mkono. Mbowe kwa sasa anahitaji mbadala hilo halikwepeki.
Kwanini mbadala? Kwa sababu ya aina ya siasa za sasa na aina ya watu aliowajenga ndani ya chama. Amejenga watu wenye uthubutu ambao kweli wanaweza kutuvusha kama Chama kitachanga karata zake vizuri.
Kwanini Mbowe asigombee awamu hii?
Ni kwasababu ya hisia ambazo tumezizoea kuwa Mbowe akigombea basi wapinzani wake ama mpinzani wake lazima wadidimizwe/adidimizwe ndani ya chama.
Mbowe akijiweka kando kisha akasimamia mchakato vizuri basi atapatikana kiongozi mzuri wa nyakati hizi na chama kitainuka tena kwa kasi ya ajabu.
Mbowe alijichanganya kwenye maridhiano hilo ni jambo lingine, wanachama wanatekwa mpaka imekuwa kwaida sasa. Kwa kweli tunahitaji mfumo mpya.
Nitaenda kwa Mbowe kumsihi chonde chonde aiangalie kesho ya CHADEMA, ajenge heshima yake kubwa kwa nyakati hizi. Ama kwa hakika nitamueleza kuwa this time kama ataamua kugombea basi amekiua chama.
Nitamuomba katu asisikilize machawa wachache wanaobweka ambao kwa kipindi hiki wameonekana dhahiri nia zao.
Nitamwambia kuwa hatusemi Mbowe must go bali tunasema kuwa Mbowe ni wakati wake sasa wa kutwaa heshima yake ndani ya chama ambayo haitafutika vizazi na vizazi.