Pre GE2025 Nitaenda kwa Mbowe kumshauri aachane na mambo ya uenyekiti safari hii. Bado tunaipenda CHADEMA tusingependa kuvuka mwaka vibaya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
chaggadema
 
Hakuna mtu yoyote CDM; narudia tena mtu yeyote ambaye anaweza kusimama na Mbowe kwa sanduku la kura CDM akatoboa.
Hii ni nadharia unayo takiwa kuifanyia majaribio ili ujue usahihi wake ulivyo. Mhimize Mbowe akachukue fomu.

Baada ya hapo tuta kutafuta urudi hapa kutupa mrejesho wa matokeo halisi. Sasa hivi unatuchosha tu na bla bla zisizo kuwa na msingi wowote.
 
Wee wee, umuachishe ULAJI ! Jamani jamani !
 
Kuna Wapumbavu ambao sio Wana CHADEMA (hawana Kadi), sio washabiki Bali ni wanafiki, wazandiki ambao wamepata platform ya kuandika at least nao waonekane wanajua kuandika.

Juzi Kati hata uchaguzi wa Serikali za mitaa hamkushiriki, Mbowe aliandamana yeye na mwanae na baadhi ya wana CHADEMA but Leo kila kenge inaijua CHADEMA, imekua mshauri...... pumbavu Kabisa
 
Hakuna mtu yoyote CDM; narudia tena mtu yeyote ambaye anaweza kusimama na Mbowe kwa sanduku la kura CDM akatoboa.

Fikisheni ujumbe, aibu itafuata tena mbaya ya kumfanya huyo mtu kupata sababu ya kukihama chama.
Mbowe anaweza kushinda kwa njia ya kura maana ana hela za kuhonga wajumbe wapiga kura, ila hana uwezo tena wa kuteka nyoyo za wafuasi wa cdm. Lipumba na CUF ni mfano halisi wa hiki nikisemacho. Mbowe akubali tu kuwa wakati ukuta.
 
Nitamwambia kuwa hatusemi Mbowe must go bali tunasema kuwa Mbowe ni wakati wake sasa wa kutwaa heshima yake ndani ya chama ambayo haitafutika vizazi na vizazi.📌🔨
 
Kama wenyeviti wa mikoa nchi nzima wameenda kumuomba mbowe agombee basi bado wanamhitaji wenye chama Chao. Ngoja tuone
Hawajaenda kumuomba, bali yeye amewaita na kuwalipa ili ionekane wanamuomba agombee tena.
 
shida yako hujiamini.
uchaguzi wa mashindano ndo demokrasia yenyewe, sasa kama hakuna ushindani mnataka lisu apite bila kupingwa?
acheni wapigakura waamue
Hakatazwi, ila miaka 20 inamtosha, alipaswa kusoma alama za nyakati.
 
Naunga mkono hoja, mimi nitaandika tuu humu asome.
P
 
Nitasema wazi kwamba siwezi kuamini kwamba Tundu Lissu atashinda uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema. Kwa maoni yangu, nafasi yake inaonekana kuwa na changamoto nyingi, na kuna maswali mengi kuhusu uwezo wake wa kuweza kuongoza chama hiki kwa mafanikio. Chadema ni chama chenye historia ndefu na kina wanachama wengi wenye maono tofauti, na ni muhimu kwa kiongozi kuweza kuunganishwa na kila mmoja wao.

Ikiwa Lissu atafanikiwa katika uchaguzi huu, nitahitaji kufikiria upya msimamo wangu kisiasa.

Nimekuwa nikihusishwa na Chadema kwa muda mrefu, lakini kama kiongozi atakayechaguliwa hawezi kuleta mabadiliko chanya, nitakuwa na sababu ya kuhama na kujiunga na CCM.

Ninatazamia kuona mabadiliko na nguvu mpya katika uongozi wa Chadema, lakini kama hali itabaki vile vile, nitajikuta katika nafasi ya kutafuta chama kingine ambacho kinaweza kufanikisha malengo yangu ya kisiasa. Hivyo basi, nasubiri kwa hamu kuona matokeo ya uchaguzi huu na athari zake kwa mustakabali wa siasa nchini.
 
Mnataka kukizamisha chama nyie,Kawashtukia 😄
Mada zimekua nyingi sana humu kila siku Mbowe,mbowe,mnalala mnaamka ni Mbowe tu

Nyie mkijitoa wanachama wapo wengine watajiunga nae
Kuna Watanzania zaidi ya Milioni 60 wapo
 
Hebu wewe unaetaka kwenda kumshauri weka namba yako ya simu hapa upigiwe simu upewe ushauri pia weka picha yako tukuone
Usidharau ushauri huu
 
Tukifanya mabadiliko sauti itaanzia ndani
 
Kwani akigombea wapigakura wakaamua kuna shida gani?.Ili demokrasia ionekane imekua lazima kuwe na ushindani sawa ili wapigakura waamue kilichobora kwao.ilimradi katiba iwe inaruhusu kulingana na sifa husika.Haya mengine mnayaleta kwania mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…